Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Waziri Libya atumbuliwa baada ya kukutana na mwenzie wa Israel
Kimataifa

Waziri Libya atumbuliwa baada ya kukutana na mwenzie wa Israel

Spread the love

KIONGOZI wa serikali ya Libya amemsimamisha kazi waziri wake wa mambo ya nje baada ya mwenzake wa Israel kutangaza kuwa, wawili hao walifanya mazungumzo mjini Rome wiki iliyopita. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea)

Waziri Mkuu, Abdulhamid Dbeibah amesema jana Jumapili katika taarifa iliyochapishwa pia kwenye mtandao wa Facebook kuwa Najla al-Mangoush amesimamishwa kazi kwa muda na atakuwa chini ya uchunguzi wa tume inayoongozwa na waziri wa sheria.

Wizara ya mambo ya nje ya Libya imeelezea kuwa mkutano huo ulikuwa sio rasmi na kwamba wawili hao walikutana bila kupanga, japo taarifa za mkutano huo tayari zimesababisha maandamano katika miji kadhaa ya Libya.

Mzozo huo wa kisiasa ulizuka jana jioni baada ya wizara ya mambo ya nje ya Israel kueleza kuwa, mawaziri wa mambo ya nje wa Israel na Misri walikutana wiki iliyopita.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa, Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Eli Cohen na Mangoush, mwenzake wa Libya, walizungumza mjini Rome katika mkutano ulioandaliwa na Waziri wa mambo ya nje wa Italia, Antonio Tajani.

Israel imeuelezea mkutano huo kama mpango wa kwanza wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Tangu mnamo mwaka 2020, Israel imekuwa ikijaribu kurejesha uhusiano wake na mataifa kadhaa ya Kiislamu kupitia mkataba maarufu kama Abraham Accords, uliosimamiwa na Marekani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

error: Content is protected !!