Saturday , 30 September 2023
Home Kitengo Michezo Mkewe Messi amkumbatia Jordi Alba kimakosa akidhani ni mumewe
Michezo

Mkewe Messi amkumbatia Jordi Alba kimakosa akidhani ni mumewe

Spread the love

BAADA ya ushindi wa timu anayochezea Lionel Messi, Inter Miami dhidi ya FC Cincinnatti kwa matuta ya penalty nchini Marekani, uwanja ulifurika kwa mbwembwe na vifijo huku kila shabiki akikimbia uwanjani kuwapongeza wachezaji wa Inter Miami. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Mkewe Lionel Messi, Antonela ni mmoja wa mashabiki wakuu wa mumewe aliyejitosa uwanjani kumpa mumewe pongezi kwa kumbatio la aina yake kwa kuiwezesha timu yake kufuzu katika hatua nyingine.

Katika video ambayo imekuwa ikienezwa mitandaoni kuanzia jana Jumapili, Antonela alionekana kuelekea uwanjani moja kwa moja na ghafla akampa kumbatio hilo matata mchezaji mwenza wa Messi ambaye pia wamekipiga naye muda mrefu kutoka enzi za Barcelona, Jordi Alba.

Mrembo huyo aliingia uwanjani muda mfupi baada ya filimbi ya mwisho kujiunga na sherehe hizo na kumtafuta mumewe ili kumpongeza.

Video iliyokuwa ikizunguka kwenye mitandao ya kijamii ilimuonyesha akidhani alikuwa amempiga macho mume wake na kuingia kumkumbatia.

Inajulikana kwamba alikosea na kuelekea kwa mchezaji  mwezie wa mumewe,​​Jordi Alba na kumkumbatia kwa mara ya kwanza kama mtu muhimu kuliko mumewe.

Antonela alibaini hitilafu hiyo na kuendelea kumkumbatia Alba nusunusu, huku wawili hao wakicheka tukio hilo la kimakosa.

Mshambulizi huyo mashuhuri alianza kutoka kwenye benchi wakati Inter Miami ilipokutana na New York Red Bulls na alianzishwa tu kwenye mechi katika kipindi cha pili.

Ripoti za mtandao wa Sportbible zimeripoti kuwa Messi aliingia akitokea benchi na kupata bao la kufutia machozi timu yake ikipata ushindi wa 2-0 na kutoka mkiani mwa Mkutano wa Mashariki wa MLS.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!