Saturday , 30 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Mnangagwa ashinda uchaguzi, upinzani wapinga
Kimataifa

Rais Mnangagwa ashinda uchaguzi, upinzani wapinga

Spread the love

TUME ya taifa ya uchaguzi nchini Zimbabwe imemtangaza Rais Emmerson Mnangagwa kuwa mshindi wa kiti cha Urais katika uchaguzi uliofanyika Jumatano 23 Agosti 2023.

Hata hivyo, upinzani umeyakataa matokeo ya uchaguzi ambao waangalizi wa kimataifa walisema pia kuwa haukukidhi viwango vya demokrasia. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kulingana na matokeo rasmi yaliyotangazwa jana Jumapili na mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi ya nchi hiyo Justice Chigumba, Rais Emmerson Mnangagwa mwenye miaka 80, ameshinda kwa kupata asilimia 52.6 ya kura dhidi ya asilimia 44 za mpinzani wake mkuu Nelson Chamisa, mwenye miaka 45.

Katika uchaguzi huo, raia wa Zimbabwe walikwenda katika vituo vya kupigia kura kuchagua rais na wabunge Jumatano na Alhamisi, katika zoezi lililotawaliwa na ucheleweshaji kitendo ambacho kilichochea shutuma za udanganyifu na ukandamizaji wa wapigakura zilizotolewa na upinzani.

Matokeo ya uchaguzi wa Rais yalipokelewa kwa nderemo na wafuasi wachache wa chama tawala katika ukumbi wa mikutano, lakini msemaji wa chama cha “Citizens Coalition for Change” cha Nelson Chamisa alisema kuwa chama hicho hakikutia saini majumuisho ya mwisho aliyoyataja kuwa ya uongo.

Alisema kuwa hawawezi kuyakubali matokeo na kwamba hivi karibuni chama hicho kitatangaza hatua inayofuata.

Akijibu madai ya upinzani, Rais Mnangagwa amesema wanaohoji matokeo ya uchaguzi wanapaswa kwenda mahakamani.

Uchaguzi wa Zimbabwe ulikuwa ukitazamwa katika mataifa ya Kusini mwa Afrika kama kipimo cha uungwaji mkono wa chama cha Mnangagwa cha ZANU-PF ambacho utawala wake wa miaka 43 umekuwa ukikabiliwa na mdororo wa uchumi na tuhuma za uongozi wa kibabe.

Mwaka mmoja baadaye, alimshinda kwa tofauti ndogo Nelson Chamisa kwa mara ya kwanza katika uchaguzi ambao viongozi wa upinzani waliulaani kuwa ulikuwa na vitendo vya udanganyifu.

Uchaguzi wa wiki hii, ulilazimika kuingia katika siku ya pili kwa sababu ya kucheleweshwa kwa karatasi za kupigia kura katika baadhi ya maeneo muhimu ikiwemo Harare, ambapo ni ngome ya upinzani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

error: Content is protected !!