Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Madiwani Msalala wamtumia ujumbe Rais Samia
Habari Mchanganyiko

Madiwani Msalala wamtumia ujumbe Rais Samia

Spread the love

MADIWANI wa Halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama, Mkoa wa Geita, wametuma ujumbe wa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kutokana na Serikali yake kuongeza fedha kwa ajili ya uimarishaji sekta muhimu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita…(endelea).


Madiwani hao wametoa pongezi hizo hivi karibuni wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo, pamoja na wakuu wa idara na vitengo, ambapo wamemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mary Mhoha, kuzifikisha kwa Rais Samia.

Madiwani hao wameipongeza Serikali ya Rais Samia, kwa kuongeza fedha kwa ajili ya kuimarisha sekta ya elimu, afya, barabara, maji na nishati ya umeme vijijini kupitia mradi wa REA, kwenye halmashauri hiyo.

Awali, hoja ya pongezi kwa Rais Samia, ilitokewa na Diwani wa Kata ya Mwakata, Sixtbert Ibrahim, kisha kuungwa mkono na madiwani wote waliohudhuria mafunzo hayo.

Sixbert alisema, hatua ya Serikali ya Awamu ya Sita kuelekeza fedha kwenye miradi mbalimbali kwenye wilaya hiyo, inatoa fursa kwa Halmashauri ya Msalala ‘kukimbia’.


Katika mafunzo hayo, Mhita alimpongeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Khamis Katimba kwa jitihada na mikakati yake aliyoionesha katika muda mchache tangu aingie kwenye halmashauri hiyo.

“Halmashauri imepata mtu makini sana, tuungane naye kuhakikisha malengo yake mapana yanafikiwa. Kwa muda mchache tumeona mwelekeo wake chanya,” alisema.

Kwenye mafunzo hayo, Mhita pia alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme kwa kukubali ombi la kutoa wakufunzi wawili kuwezesha mafunzo hayo kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kusimamia miradi ya maendeleo.

Madiwani hao walimpongeza mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mibako Mabubu na mkurugenzi wake (Katimba), kwa kuwezesha mafunzo hayo pamoja na mambo mengine, yalilenga viongozi hao kujua mipango ya bajeti ya halmashauri inayopanga hivyo kuwa rahisi kwao kufanya ufuatiliaji katika ngazi mbalimbali.

“Ninawaomba waheshimiwa madiwani kutokukubali vyanzo vya mapato kutoroshwa katika maeneo yenu ya utawala,” alisema Katimba.

Katibu Tawala wa Wialaya hiyo, Mohamed Mbega amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni ili kulinda heshima na maadili ya uongozi.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Abdallah Urari amewaomba viongozi hao kutoa ushirikiano kwa maafisa wa taasisi hiyo.

Alisema kwamba, taasisi hiyo ina mpango wa kutembelea kata zote kwa ajili ya kuanzisha huduma ya TAKUKURU RAFIKI, yenye lengo la kuongeza uwajibikaji na utoaji huduma bora kwa jamii na kutatua changamoto.

Hata hivyo alisema, taarifa za udanganyifu katika ukusanyaji mapato na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo kwa baadhi ya wataalamu na viongozi wa halmashauri hiyo pamoja na ‘upigaji’ kwa madiwani, zipo mezani kwake, ameonya tabia hiyo na kuahidi kufanyia kazi taarifa hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!