URUSI imesitisha mashambulizi katika miji mingi zaidi ya nchini Ukraine leo tarehe 7 Machi, 2022 ili kuruhusu raia kuondoka, Anaripoti Mwandishi wetu …(endelea).
Usitishaji huo wa mapigano utafanyika kuanzia saa 10:00 jioni kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi huku njia za uokoaji zikiwekwa katika mji mkuu wa Kyiv, Kharkiv, Mariupol na Sumy.
Miji yote hii kwa sasa iko chini ya operesheni kubwa ya uvamizi wa Urusi, licha ya kwamba maofisa wa Ukraine bado hawajathibitisha hili.
Mwishoni mwa wiki juhudi za kufungua njia ya kuruhusu raia kuondoka Mariupol Kusini Mashariki mwa nchi hiyo zilisambaratika.
Maofisa wa Ukraine wanasema hili ni sababu ya Urusi iliendelea kushambulia mji huo wakati wa saa zilizokubaliwa za kusitisha mapigano.
Leave a comment