MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema wanatarajia kujenga shule za sekondari za ghorofa 20, ili kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan, la ujenzi wa shule hizo ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa ardhi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Makalla ametoa taarifa hiyo leo Jumatatu, tarehe 7 Machi 2022, akitoa salamu za wananchi wa Dar es Salaam, katika ziara ya Rais Samia kwenye Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa, jijini humo.
“Lakini kwa Dar es Salaam umeshatoa maelekezo kuwa, ardhi haitoshi tuendelee kuangalia namna ya kujenga maghorofa na sisi hizi fedha ulizotoa tunazielekeza kwenye maghorofa, tunajenga maghorofa 20,” amesema Makalla.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema wamepokea Sh. 15 bilioni kutoka serikalini ambazo zimetumika kujenga madarasa 747.
“Tunajifuzna mwakani tuwe na matokeo mazuri ili kusiwe na changamoto ya madarasa na uandikishwaji umekwenda vizuri kidato cha kwanza ni asilimia 94 ambao wamjeiunga na shule ya msingia ni asilimia 95,”amesema Makalla.
More Stories
Tume ya Ajira yataja sababu vijana kukosa ajira
Hazina yaendelea kuongoza moko darasa la saba, Yaongoza Kinondoni mfululizo,
Tanzania ya kidijitali: Kuwekeza kwa vijana ni kuwekeza katika mustakabali sahihi