KUNDI la wanaharakati huko Urusi limeripoti kwamba padre ambaye alitoa mahubiri ya kupinga vita nchini Ukraine Jumapili, amekamatwa na anatarajiwa kufunguliwa mashtaka leo tarehe 7 Machi, 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)
Mwandishi wa BBC nchini Urusi, Andrey Zakharov ameripoti kuwa padre John Burdin aliwekwa chini ya ulinzi muda mfupi baada ya kutoa mahubiri katika kanisa dogo kwenye kijiji cha Karabanovo.
Padre huyo alihubiri dhidi ya vita akiwaelezea wananchi kile kinachoendelea nchini Ukrenia akiwaonesha picha za matukio ya vita.
Polisi nchini Urusi wamemfungulia mashtaka ya kudharau kazi za jeshi, kosa la jinai ambalo limeanzishwa na Serikali ya Urusi wiki iliyopita.
Tangu kuanza kwa vita nchi Ukrenia kumekuwa na vizuizi vingi kwa wanaharakati nchini Urusi ambapo pamoja na kujua athari bado maelfu ya watu wameendelea kuandamna barabarani katika miji mingi kupinga vita hivyo.
Zaidi ya watu 13,000 wameshakamatwa wakiwemo 4,600 waliokamatwa Jumapili.
Leave a comment