RAIS wa Kenya William Ruto amesema kwamba hatakubali “kutoijali nchi” baada ya maandamano ya ghasia kukumba mji mkuu, Nairobi na mji wa magharibi wa Kisumu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea)
Maandamano hayo yaliandaliwa na mwanasiasa wa upinzani Raila Odinga ambaye analaumu sera za serikali kwa kuzidisha kupanda kwa gharama ya maisha.
Pia amedai bila ushahidi kwamba alishinda uchaguzi wa urais wa mwaka jana.
“Nitahakikisha kama rais kwamba nchi hii inaongozwa na sheria, na hakuna chochote zaidi ya sheria na katiba kitakachokuwa sehemu ya kile tunachofanya,” Ruto amesema.
Rais amemshutumu Odinga kwa kujaribu kuanzisha mgogoro kwa mara ya pili, akisema alifanya vivyo hivyo baada ya uchaguzi wa 2017 na kumlazimisha Rais wa wakati huo Uhuru Kenyatta kufikia makubaliano ambayo yalimpa mapendeleo ya serikali.

Hata hivyo, Odinga amekanusha madai hayo katika maandamano hayo mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi huku polisi wakikabiliana na waandamanaji katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Maelfu ya watu wameitikia wito wa maandamano ya kitaifa ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga, ambaye anadai kuwa uchaguzi uliopita wa Kenya uliibiwa.
Odinga, ambaye amewania urais mara tano, pia anashutumu serikali kwa kukosa kuwasaidia Wakenya kukabiliana na hali ya “kupanda” kwa gharama ya maisha.
Kuna ripoti kwamba polisi walirusha mabomu ya machozi kwa msafara wa Odinga siku ya Jumatatu.
Leave a comment