Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia atoa tahadhari mfumuko wa bei
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atoa tahadhari mfumuko wa bei

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametahadharisha uwepo wa mfumuko mkubwa wa bei nchini unaosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta duniani kutokana na vita inayoendelea kati ya Ukraine na Urusi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Rais Samia ametoa tahadhari hiyo leo tarehe 8 Machi 2022, katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Maisara Visiwani Zanzibar.

Mkuu huyo wa nchi amesema jinsi mafuta yanavyopanda bei, Tanzania haitanusurika kwani bidhaa zote zitapanda bei.

“Bidhaa zitapanda bei, nauli zitapanda bei, kila kitu kitapanda, thamani ya kila kitu itapanda kwasababu mafuta yanapanda bei,” amesema Rais Samia.

Aidha amesema kuna minong’ono imenza kusikika kuwa maisha yamekuwa magumu huku lawama zikipelekwa kwa viongozi kuwa hawana baraka.

“Si baraka ya kiongozi, ni hali ya ulimwengu inavyokwenda mafuta yanapanda bei duniani na bidhaa zote zitapanda bei,” amesisitiza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!