Saturday , 18 May 2024
Home Habari Mchanganyiko RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu
Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love

 

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya Kanda ya Kati Dodoma imekabidhi silaha mbili za moto kwa RPC Dodoma zilizokamatwa kwenye operesheni zilizofanyika tarehe 24 hadi 28 Aprili,2024 mkoani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, leo tarehe 03 Mei, 2024 katika ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Kaimu Kamishna Msaidizi Kanda ya kati, Mzee Kasuwi amesema, silaha hizo aina ya gobore zilikuwa zinamilikiwa na Hamisi Chambo (46) na Abdilah Juma (45) wote wakazi wa kata ya Segera na zilikuwa zikitumika kulinda mashamba ya bangi.

Aidha, kamishna Kasuwi amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwa kupiga simu bure kupitia namba 119.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma (RPC) Theopista Mallya ameishukuru Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kutokomeza uhalifu na kutoa rai kwa wananchi kufuata sheria za nchi na taratibu zake kwani Jeshi la polisi lipo na litaendelea kutokomeza matumizi ya dawa za kulevya.

Silaha zilizokabidhiwa, zilikamatwa katika operesheni iliyofanyika maeneo ya wilaya ya Chamwino na Dodoma mjini ambapo jumla ya ekari 9.5 za mashamba ya bangi ziliteketezwa, kilogramu 156.23 za bangi na misokoto 127 ya bangi zilikamatwa ambapo watuhumiwa 16 wanashikiliwa kuhusika na dawa hizo .

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Lissu akabidhiwa gari lake, aomba msaada wa matengenezo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu leo Ijumaa amekabidhiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

error: Content is protected !!