Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mrithi wa Maalim Seif atema cheche
Habari za SiasaTangulizi

Mrithi wa Maalim Seif atema cheche

Spread the love

 

MWENYEKITI mpya wa chama cha upinzani nchini Tanzania-ACT Wazalendo, Juma Duni Haji maarufu Babu Duni amewashukuru wote waliomchagua kushika wadhifa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Babu Duni amechaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa ACT-Wazalendo uliofanyika jana Jumamosi, tarehe 29 Januari 2022, kwa kura 339 sawa na asilimia 73.06 ya kura zote 468.

Mshindani wake wa karibu alikuwa waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akipata kura 125 sawa na asilimia 26.

Babu Duni amechukua nafasi iliyoachwa wazi na mkongwe mwenzake wa siasa hususan Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alifariki dunia tarehe 17 Februari 2021, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Baada ya kutangazwa mshindi, Babu Dunia alizungumza na wajumbe wa mkutano huo na kuelezea anachokwenda kukifanya.

Fuatilia hotuba yake yote aliyoitoa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Wanaotaka kujifunza ZEC kwao kukoje?

Spread the loveMKURUGENZI wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Thabit Idarous...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Biteko, Nape wanadanganya?

Spread the loveKWA mila na desturi zetu za Kiafrika mkubwa huwa hakosei,...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miamka 60 ya Muungano: Tunakwama wapi?

Spread the loveRAIS wa Jamhuri, Samia Suluhu Hasssan, Ijumaa iliyopita, aliongoza mamilioni...

error: Content is protected !!