Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Chana atoa maagizo kiwanga cha sukari Mkulazi
Habari za Siasa

Waziri Chana atoa maagizo kiwanga cha sukari Mkulazi

Spread the love

 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge na Uratibu nchini Tanzania, Balozi Pindi Chana amemtaka mkandarasi anayesimamia kazi ya ujenzi Kiwanda cha Sukari Mkulazi kilichopo Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro kukamilisha ndani ya muda uliowekwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Aidha, ameelekeza bodi ya kiwanda pamoja na wataalamu kuweka bima kwa ajili ya Kiwanda cha Sukari Mkulazi.

Balozi Chana ametoa maagizo hayo jana Jumamosi, tarehe 29 Januari 2022, alipotembelea kiwanda cha hicho kwa lengo la kujionea maendeleo na hatua ya ujenzi zilipofikiwa.

“Tunahitaji kuendeleza ushirikishwaji wa ujenzi wa kiwanda kwa sababu wananchi waliozunguka eneo la ujenzi wa kiwanda wanamatumaini makubwa,” alisema Balozi Chana.

Alisema kiwanda hicho kikianza kazi kitapunguza tatizo kubwa la uhitaji wa sukari nchini na tunapaswa kuzalisha sukari nyingi ya kutosha ili kuwezesha mahitaji ya ndani na nyingine kusafirsha nje ya nchi.

“Ni lazima turatibu kwa pamoja ili kiwanda hiki cha sukari kianze kufanya kazi mwezi wa nane,” alisisitiza Balozi Chana

Waziri huyo, alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia ujenzi wa kiwanda hicho.

“Ipo tija ya uwepo wa kiwanda hiki na kuna ‘Political will’ ipo hivyo bodi na wataalamu kujipanga kuona ujenzi unakamilka kwa wakati,” alisisitiza.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya kiwanda hicho, Dk. Hildelitha Msita alisema mradi huo ni mradi mkubwa na una matarajio makubwa kwa Taifa, “tutasimamia mradi huu kwa mujibu wa muda wa mkataba uliowekwa na hakutakuwa mabadiliko ya muda.”

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge na Uratibu nchini Tanzania, Balozi Pindi Chana

Awali, akitoa taarifa, Mkurugenzi Mtendaji wa Mkulazi, Selestine Some alisema maeneo mbalimbali ya ujenzi wa kiwanda yapo katika hatua ya msingi na wameanza kupandisha vyuma kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kiwanda ambayo itaenda pamoja na kufunga baadhi ya mitambo ya kiwanda.

“Mpaka sasa tumepokea kontena 63 za vifaa vya viwanda na tunatarajia kupokea kontena 450 kwa supplier wa mitambo ya kiwanda,” alieleza Selestine

Kwa upande wake, Mkandarasi Msaidizi, John Bura alisema ujenzi wa kwanda hicho wanashirikiana na Mkandarasi Mkuu kumaliza mradi kwa wakati kwa kuhakikisha wanaongeza nguvu kazi kwa kuongeza rasilimali watu na kazi inafanyika saa 24.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!