Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Mr Eazi, DJ Edu kuachia ngoma mpya ya Wena
Burudika

Mr Eazi, DJ Edu kuachia ngoma mpya ya Wena

Spread the love

BAADA ya kutangaza habari kubwa za ujio wa project ya Afrodance Soundsystem, wasanii wakubwa wa muziki, Mr Eazi na DJ Edu wameachia ngoma ya kwanza kwenye project hiyo iitwayo Wena ambao pia umemshirikisha mwanamuziki wa Afrika Kusini, Ami Faku. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mr Eazi amenukuliwa akisema, “Narudi kule nilipoanza, nitafanya tamasha kubwa kwenye vyuo vikuu,” na kuongeza, “Huko ndiko nilipoanzia kuimba.

Natarajia kwa furaha kubwa kuanza safari hii mpya, na nina shauku kubwa ya kuona muziki mzuri ukianza kutoka na kusindikizwa na uzoefu wake wa moja kwa moja.”

Wimbo huu uliotolewa na Choplife Limited April 28 Aprili, unaonyesha jinsi Afrodance mpya ilivyosukwa na DJ Tárico ambayo ni mwendelezo wa kazi za Amapiano za Eazi katika nyimbo zake za hivi karibuni.

Ndani yake ameshirikishwa Ami Faku, mmoja kati ya wasanii wanaosikilizwa zaidi nchini Afrika Kusini, ambaye anatoa ujumbe wenye kugusa moyo kwa lugha ya Xhosa, huku Eazi akijibu kwa Kiingereza.

Ujumbe uliomo ni hadithi ya wapenzi wanaotaka kuwa pamoja lakini hawajapata kufikia malengo yao, ambayo ni janga ambalo linaweza kutatuliwa tu kwa kuchezwa jukwaani.

Wena utaachiwa rasmi tarehe 28 Mei 2023 ikiwa katika mkusanyiko uliopewa jina la ‘Choplife Vol. 1: Mzansi Chronicles’ ambapo wameshirikishwa wazalishaji muziki maarufu na ma-DJ wa kiwango cha juu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

error: Content is protected !!