Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Sakata kuzima taa Taifa: Vigogo wasimamishwa, mechi za usiku zapigwa ‘stop’
Michezo

Sakata kuzima taa Taifa: Vigogo wasimamishwa, mechi za usiku zapigwa ‘stop’

Spread the love

 

VIONGOZI wanaosimamia Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa sakata la kuzima kwa taa katika Uwanja huo wakati mechi zikichezwa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taa hizo ziliwahi kuzimika katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), uliochezwa kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Timu ya Taifa ya Uganda (Uganda the Cranes), lakini pia jana Jumapili zilizimika tena kwa muda wakati Klabu ya Yanga na Rivers United kutoka Nigeria, wanacheza mechi ya robo fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Elwuteri Mangi, Waziri wa Wizara hiyo, Balozi Pindi Chana ameagiza viongozi wa Uwanja huo akiwemo, Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Salum Mtumbuka.

Mbali na Mtumbuka, Balozi Chana amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamuduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu, kumsimamisha kazi Mhandisi wa Uwanja huo, Manyort Kapesa na Afisa Tawala, Tuswego Nikupata.

Mbali na utenguzi huo, Yakubu amemteua Mlinde Mahona, kuwa Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa, kuanzia tarehe 1 Mei 2023.

Aidha, Yakubu ameagiza mechi zitakazochezwa katika Uwanja huo zichezwe jioni badala ya usiku, wakati Wizara inakamikisja taratinu za Kupata mzabuni atakayefabya ukarabatu mkubwa katika Uwanja huo kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa Michuano ya kimataifa.

“Ameagiza mamlaka za nje ya wizara kufanya uchunguzi wa kukatika unene katika Uwanja huo na hatua za kuchukua,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!