Monday , 6 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Matende, mabusha tishio Kinondoni, wananchi waitwa kupata kinga tiba
AfyaHabari Mchanganyiko

Matende, mabusha tishio Kinondoni, wananchi waitwa kupata kinga tiba

Spread the love

MAGONJWA yasiyopewa kipaumbele ya Mabusha na Matende, bado yanaendelea kusumbua kata 10 za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, kutokana na kuwepo kwa maambukizi mapya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamebanishwa leo tarehe 12 Machi 2024, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akielezea tathimini iliyofanywa na Serikali kuhusu magonjwa hayo kati ya Agosti 2023 na Februari 2024.

Ummy ametaja kata hizo kuwa ni, Tandale, Kijitonyama, Mwananyamala, Kigogo, Mzimuni, Magomeni, Ndugumbi, Hananasif, Kinondoni na Makumbusho.

“Katika Jiji la Dar es Salaam hakuna maambukizi mapya ya ugonjwa matende na mabusha, isipokuwa tumebakiwa na Manispaa ya Kinondoni. Tathimini tumefanya Kinondoni katika kata 10 hazina maambukizi mapya lakini tumebakiwa na kata 10 na tathimini imeonesha bado zina maambukizi mapya kwa kiwango cha asilimia 2.5,” amesema Ummy.

Amesema Serikali kwa kushirikiana na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, itaendesha zoezi la utoaji kinga tiba kwa wananchi wa kata hizo, ndani ya muda wa miaka miwili.

“Nitoe wito kwa wananchi kushiriki katika kampeni ambazo tuanziendesha katika kata 10 za mkoa wa Dar es Salaam za kutoa kinga tiba. Hizi kinga ni salama na natoa wito jitokezeni msiogope watalaamu wataendeleza dawa hizi ni salama hazina madhara yoyote,” amesema Ummy.

Aidha, Ummy amesema maambukizi mapya ya matende yamepungua katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, kutoka halmashauri 119 kati ya 184 zilizokuwa na maambukizi hadi kufikia halmashauri saba.

Ummy amesema zoezi la utoaji kinga riba ya matende na mabusha, imesitishwa katika maeneo ambayo hayajaripotiwa kuwa na maambukizi mapya, huku akiwataka wananchi kuendelea kujikinga ili wasiambukizwe.

Pia, Ummy amewataka wagonjwa wa matende na mabusha, kwenda hospitali kufanyiwa upasuaji kwa kuwa hakuna gharama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari Mchanganyiko

Tanzania  yasisitiza kuwa Kituo Kikuu cha Uchimbaji Madini Afrika

Spread the loveTanzania imeendelea kusisitiza adhma yake ya kuwa kituo kikuu cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

error: Content is protected !!