Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, waandishi wa habari ngoma nzito
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe, waandishi wa habari ngoma nzito

Spread the love

Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi kesho inatarajia kutoa uamuzi wa kukubali ama kuyakataa maombi ya Freeman Mbowe ya kutaka waandishi wa habari wanaodai mtoto wake Sh milioni 62.7 wamlipe gharama. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Maamuzi hayo yametolewa leo Machi 12, 2024 na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Mary Mrio katika kesi iliyofunguliwa na Mbowe dhidi ya waandishi wa habari 10 wanaomdai mtoto wake, Dudley Mbowe ambaye ni Mkurugenzi wa gazeti la Tanzania Daima.

Kupitia wakili wake John Mallya Mbowe aliwasilisha maombi mahakamani akitaka nyumba iliyokamatwa na dalali kwa amri ya mahakama iondolewe na wajibu maombi wamlipe gharama za kesi.

Waandishi wa habari 10 wanamdai Mkurugenzi wa Tanzania Daima, Dudley Mbowe Sh milioni 62.7 wameachia nyumba ya Freeman Mbowe waliyoikamata ili kuipiga mnada lakini wamegoma kulipa gharama za kesi kwa sababu hata wao wanaingia gharama katika kudai haki yao.

Kulwa Mzee kwa niaba ya wajibu maombi alidai walipitia nyaraka zote na viambatanisho wamejiridhisha na wamekubaliana kwa pamoja kwamba hiyo nyumba waliyoikamata ni ya familia lakini inamilikiwa na Freeman Mbowe.

“Mheshimiwa tumepitia nyaraka pamoja na viambatanisho ikiwemo hati ya nyumba, tumejiridhisha kwamba mkurugenzi tunayemdai Dudley Mbowe si mmiliki, hivyo tunaiomba Mahakama tuiondoe hiyo nyumba kwenye maombi yetu.

“Kuhusu gharama mheshimiwa, kwa uelewa wetu kwa mashauri ya migogoro ya kikazi hakuna gharama na hiyo inatokana na uwezo wa vipato vidogo vya wafanyakazi.

“Wakati sisi tunafanya hili jambo tulikuwa tukiamini kabisa kuwa ni nyumba ya mkurugenzi wetu kwa sababu katika hatua ya makubaliano alikuwa anatuambia kuwa tutafanya vikao nyumbani kwake na tumefanya hapo vikao kwenye hiyo nyumba,” alidai Kulwa.

Akijibu dalali wa Mahakama Jesca Massawe alidai alipokea amri ya Mahakama kwa ajili ya kukamata nyumba hiyo.

“Sisi kama madalali wa Mahakama katika kutekeleza majukumu yetu, tulikaa na Mahakama hii chini ya Jaji Mfawidhi akatuelekeza kuwa katika mashauri haya ya kukamata mali tusijihusishe na utambuzi wa mali bali tukamate na kama kuna changamoto basi italetwa mahakamani,” alidai na kuongeza kwamba alitekeleza amri ya Mahakama kama ilivyoelekezwa.

2 Comments

  • Huyo hakimu naye anatakiwa achukuliwe hatua za kinidhamu. Unakamataje nyumba bila kujua mmiliki wake? Kama alikuwa ni mpangaji je?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!