KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi, Sauti ya Watanzania, kimesema kimechagua kukiunga mkono Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kuwa kina nia ya dhati kutatua matatizo ya wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).
Sababu hiyo imetajwa leo tarehe 27 Aprili 2024, na mwanachama wa kikundi hicho, Boniface Mwabukusi, akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu, uliofanyika mkoani Singida.
“Tunaiunga mkono Chadema kwa sababu ya namna inavyojiweka, hata watoto wanalia njaa unaangalia nani anayelia sana ndiyo mwenye njaa. Tunaiunga mkono Chadema kwa sababu kazi kubwa wanayofanya. Chadema ndiyo chama pekee utakuta kina wanachama ambao wanatumia gharama zao kujenga demokrasia,” amesema Mwabukusi.
Akizungumzia maandamano yanayofanywa na Chadema maeneo mbalimbali, Mwabukusi amesema yanafanyika kwa wakati sahihi kwa kuwa yanalengo la kudai katiba mpya itakayoleta mgawanyo wa madaraka kati ya Bunge, mahakama na Serikali.
Leave a comment