Friday , 24 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki
Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the love

Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Serikali ya Watu wa Zanzibar (PBZ). Arafat amehudumu kama Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) tangu Juni 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kabla ya kuteuliwa kuwa bosi wa ZIC na Rais Mwinyi, aliwahi kuwa mhasibu katika Benki ya Exim jijini Dar es Salaam, akisimamia shughuli za benki hiyo nchini Tanzania, Comoro, Djibouti na Uganda.

Akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 15 katika sekta ya benki, uteuzi wa Arafat katika nafasi mpya ndani ya PBZ unamfanya kurejea katika kazi yake ya benki.

Anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Dk. Muhsin Masoud kama mkuu wa benki hiyo yenye makao yake makuu Visiwani Zanzibar.

Dk. Masoud anasifika kwa kuisimamia benki hiyo katika kipindi cha ukuaji mkubwa wa wake na kuifikisha kwenye daraja la juu tangu ilipochukua madaraka mwaka 2021.

Mwaka jana pekee, benki ilitengeneza faida kwa asilimia 44 ya mali zote sawa na Sh 2.05 trilioni, na hivyo kuimarisha nafasi yake kama moja ya benki 10 bora zaidi nchini Tanzania.

Katika ZIC, Arafat alisaidia kampuni hiyo ya bima ya serikali kuzidi kujitanua upande wa Tanzania Bara na kuanzisha huduma mpya za bunifu.

Anatarajiwa kuongoza upanuzi wa PBZ zaidi ya msingi wake wa Zanzibar kwa kufungua matawi zaidi Tanzania Bara.

PBZ imekuwa ikitaka kupanua shughuli zake hadi Tanzania Bara, kwa kuwa inafanya biashara mbali na soko lake la asili katika visiwa vya Bahari ya Hindi.

Benki hiyo ilizindua tawi jipya katika jiji la Dodoma Desemba mwaka jana na kutangaza mipango ya kupanua mtandao wake katika miji na majiji mengi zaidi ya Tanzania Bara mwaka huu.

PBZ ina vituo 45 vya huduma, huku vituo 11 vikiwa Tanzania Bara na vingine 34 vikiwa Zanzibar.

Kwa sasa benki hiyo inaajiri takriban watu 500. Kwa kawaida mashirika ya serikali ya Zanzibar ni mara chache yanatoka nje ya visiwa hivyo na yanapofanya hivyo hupata mafanikio kiduchu.

Arafat alisomea masuala ya benki na fedha katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na ana Shahada ya Uzamili (MBA) katika teknolojia ya habari kutoka Chuo Kikuu cha Coventry.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko awataka makatibu mahsusi kujiendeleza, kuwa kielelezi cha huduma bora

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Michezo

Endelea kubashiri na Meridianbet, Ligi bado zipo

Spread the love BAADA ya ligi mbalimbali kutamatika, bado kuna ligi mbalimbali...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

GGML inavyookoa walemavu dhidi ya dhana potofu

Spread the loveMKOA wa Geita ni mmoja wa mikoa ya Kanda ya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Tanzania kufungua vituo 100 vya kufundisha Kiswahili nje

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania imepanga kufungua vituo 100 vya kufundisha lugha...

error: Content is protected !!