Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kamati Kuu Chadema kuketi Mei 11
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kamati Kuu Chadema kuketi Mei 11

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), inatarajiwa kuketi katika makao makuu ya chama hicho, Mikocheni, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 11 Mei 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 9 Mei 2024 na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema, John Mrema

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, masuala matatu yanatarajiwa kuteka kikao cha kamati hiyo, ikiwemo taarifa ya uchaguzi katika ngazi mbalimbali za chama hicho.

“Kamati Kuu itakuwa na mambo yafuatayo, kupokea taarifa ya chaguzi katika ngazi mbalimbali za chama, kupokea tathimini ya maandamano ya awamu ya kwanza ya mikoa  katika wiki ya maandamanona kuweka mwelekeo wa awamu ya pili ya maandamano,” imesema taarifa ya Mrema.

Suala lingine litakalofanyiwa kazi kwenye kikao hicho ni kufanya usaili na kuteua wagombea nafasi mbalimbali katika chaguzi za kuwatafuta viongozi wa kanda nne za Chadema,  Nyasa, Serengeti, Victoria na Magharibi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!