Monday , 20 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mpina awavaa mawaziri wanaompelekea majungu Rais Samia
Habari za SiasaTangulizi

Mpina awavaa mawaziri wanaompelekea majungu Rais Samia

Luhaga Mpina
Spread the love

MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amewataka baadhi ya mawaziri aliodai kuwa wanampelekea majungu Rais Samia Suluhu kuhusu wabunge wanaokosoa utendaji wa serikali yake, waache mara moja kwani lengo la wawakilishi ni kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mpina ametoa kauli hiyo leo tarehe 10 Mei 2024, akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji,kwa mwaka wa fedha wa 2024/25, bungeni jijini Dodoma.

“Na hapa niseme kidogo kwa wale mawaziri ambao baadae hapa wakiona wameshindwa kujibu maswali yetu wanasema ooh unajua ana jambo lake, nataka tuwaambie kwamba hakuna jambo lolote tuna jambo moja tu la watanzania kupata maendeleo,” amesema Mpina na kuongeza:

“Hakuna hiyana yoyote na huko wanakopeleka majungu wajue kwamba wengine ndio tumekulia kule, kwa makamo wa Rais na leo ndio rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nimekaa pale mimi miaka mitatu na nilitoka pale kwa kuvikwa nishani.”

Akitoa maoni yake kuhusu wizara hiyo, Mpina amempongeza Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari za SiasaKimataifa

Kiongozi Mkuu Iran amteua mrithi wa Rais Ebrahim

Spread the loveKiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei,...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

error: Content is protected !!