Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv
Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the love

JESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia kuuchukua mwili wa aliyekuwa mpiga picha wa televisheni mtandao ya Ayo Tv, Noel Mwingira maarufu kama Zuchy, likisema sio za kweli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Tuhuma hizo ziliibuliwa jana asubuhi baada ya ajali ya pikipiki iliyoondoa maisha ya Zuchy, kutokea maeneo yta Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam, ambapo ilidaiwa tangu tukio hilo lilipotokea majira ya saa nane usiku Polisi walikawia kufika licha ya kupewa taarifa. Inadaiwa Polisi walisema gari lao halina mafuta.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda David Misime, Polisi hawakupewa taarifa mapema kama tuhuma hizo zinavyodai, bali walipata taarifa majira ya 10.00 alfajiri, kisha Polisi waliokuwa kwenye majukumu katika mkesha wa tamasha la Shangwe la Utawala lililokuwa linafanyika eneo la Tanganyika Packers walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupelekea Hospitali ya Mwananyamala.

Kamanda Misime amesema Polisi waliofika eneo la tukio walifanya uchunguzi na kubaini marehemu Zuchy alipata ajali ya pikipiki aliyokuwa amepanda yenye namba MC 436 CMU iliyokuwa inaendeshwa na dereva ambaye alipata majeraha na anaendelea na matibabu.

“Endapo kuna mwenye taarifa tofauti na si za uzushi au uongo kama hizo zinazosambazwa azifikshe kwa viongozi ili zifanyiwe kazi na hatua zichukuliwe,” amesema Kamanda Misime.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafugaji kuku Ihemi wanufaika na mafunzo

Spread the loveWADAU  wa mnyororo wa thamani katika sekta ndogo ya kuku...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaainisha mpango wa kusaidia wachimbaji wadogo

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameainisha mpango wa Serikali wa...

error: Content is protected !!