Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bashiru Ally aivaa serikali kukalia vibali vya wahadhiri
Habari za SiasaTangulizi

Bashiru Ally aivaa serikali kukalia vibali vya wahadhiri

Dk. Bashiru Ally
Spread the love

MBUNGE wa kuteuliwa, Dk. Bashiru Ally amesema vikwazo vinavyoendekezwa na tume ya utumishi wa umma katika kuidhinisha vibali vya wahadhari kupanda vyeo, vikwamisha vyuo vikuu nchini kuwa vya kimataifa.

Pia ameitaka serikali ipeleke marekebisho ya sheria ya utumishi wa umma bungeni kwani inagusa maeneo ya usimamizi wa rasilimali katika taasisi nyeti na za kimkakati kama vyuo vikuu vya umma. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema sheria hiyo ikibadilishwa itavipa mamlaka vyuo vikuu chini ya uongozi wa serikali kuajiri, kufanya tathmini ya utendaji wa watumishi wake, kupandisha vyeo, kusimamia nidhamu na kupima utendaji wa watumishi wao.

Akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya elimu, sayansi na teknolojia iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma jana, Bashiru ametoa mfano kuwa mwaka 2018 kuna mhadhiri mwenzake alipandishwa cheo kuwa mhadhiri mwandamizi na Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), lakini cha ajabu hadi mwaka 2021 tume ya utumishi ndipo ilipotoa kibali cha kupanda cheo hicho.

“Alikuwa amepewa barua na chuo kilichomtambua kwa sababu unapanda cheo kwa kigezo cha machapisho pamoja na uzoefu wa miaka mitatu. Chuo kikuu kikampa barua ya kutambua cheo chake, kikapeleka utumishi kwa ajili ya kibali, kibali chake kilitoka mwaka 2021 baada ya miaka mitatu.

“Huku kakaa miaka mitatu kupata cheo hicho kwa vigezo na muongozo wa chuo, lakini kibali cha kutambua cheo hicho kikatoka baada ya miaka mitatu, kwa hiyo akapata mshahara wa cheo alichokipata baada ya miaka mitatu na akalipwa mshahara wa miaka mitatu kwa cheo cha zamani.

“Wakati utumishi wanatoa kibali hicho alikuwa ametimiza vigezo kupanda nafasi ya kuwa profesa mshiriki. Kwa hiyo kibali kinakuja amepanda vyeo viwili. Tangu 2021 hadi sasa kibali cha kutambua uprofesa wake mshiriki hakijatoka. Hii maana yake tunataka vyuo viwe vya kimataifa kweli? Alihoji Bashiru.

Bashiru ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu wa CCM na Katibu Mkuu Kiongozi, alisema utumishi wanaendekeza urasimu huo ilihali takwimu zinazonesha kuna uhaba wa maprofesa na maprofesa washiriki.

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji mst. Hamisa Kalombola.

“Hili ni tatizo kubwa, kwanza linavunja moyo kwa sababu kuchapisha ni kazi ngumu sana, ni ghali na wakati mwingine gharama zinatoka mfukoni mwa anayechapisha, kwa sababu ya uhaba wa rasilimali. Lakini sherehe kubwa ni mtu anapopanda nafasi baada ya kuchapisha na kimataifa tunatambuliwa kwa kuwa na machapisho yenye hadhi,” alisema.

“Kwa hiyo yapo matatizo ndani ya vyuo lakini hata wakiyarekebisho vipo vikwazo ndani ya utumishi,” alisema.

Alisema hata waraka namba moja uliotolewa Agosti mwaka jana na Msajili wa hazina kuhusu kuyapa uhuru mashirika na taasisi nyeti, hautotekelezeka kama sheria ya utumishi wa umma haitabadilishwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chongolo atangaza ‘vita’ kwa wanaovusha wageni kinyemela

Spread the loveKATIKA kulinda usalama wa nchi kupitia mpaka wa Songwe, Mkuu...

error: Content is protected !!