Monday , 20 May 2024
Home Kitengo Biashara Wafugaji kuku Ihemi wanufaika na mafunzo
BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafugaji kuku Ihemi wanufaika na mafunzo

Spread the love

WADAU  wa mnyororo wa thamani katika sekta ndogo ya kuku wameonesha kuridhishwa  na  mafunzo ya ufugaji kuku kisasa yanayotolewa Kituo cha SilverLands Tanzania Limited (T-PEC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa (endelea).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau katika mnyororo wa thamani wa mazao ya kuku wameelezea namna sekta hiyo inavyochangia katika kuzalisha ajira sambamba na kutoa mchango chanya katika kukuza uchumi wa Taifa.

Wafugaji hao wamesema mafunzo hayo yataenda kutatua changamoto zinazoikabili tasnia hiyo  ikiwa ni  pamoja na ukosefu wa ujuzi na utaalam wa ufugaji.

Michael Nyagawa ambaye ni mfugaji mdogo wa kuku mkoani Njombe  na mnufaika wa mafunzo hayo  mbali ya kukipongeza kituo hiko  ambacho ni miongoni wa wabia wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo  Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania (SAGCOT) ameishukuru Serikali  ya awamu ya sita  chini ya uongozi  wa Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa kuweka mazingira rafiki  yanayovutia uwekezaji  nchini.

Kwa upande wake Ofisa Mwandamizi wa T-PEC, Alice Tendega amesema kituo hiko cha mafunzo kilianzishwa mwaka 2016 lengo  likiwa ni kutoa mafunzo ya kuku kwa kina na kwa muda mfupi ili kuwainua wafugaji wadogo wadogo na mashirika yasiyo ya kiserikali.

“Hadi sasa zaidi ya wanafunzi 3,500 wamepatiwa mafunzo katika fani tatu, ufugaji bora wa kuku wa nyama, ufugaji bora wa kuku wa mayai na namna bora ya ufugaji na uzalishaji wa kuku kwa ujumla.

Tunaendelea kutoa mafunzo haya kila mwaka, na hata kuongeza vituo vingine kulingana na uhitaji.” Alibainisha Tendega na kuongeza kuwa lengo lao ni kuzalisha vifaranga vya kutosha kwa ajili ya soko la ndani na la nje ya nchi sambamba na  uzalishaji wa chakula bora  cha kuku.

Naye   Meneja wa SAGCOT Kongani ya Ihemi, Khalid Mgaramo amesema bado wafugaji wengi wa kuku wanafuga chini ya kiwango kutokana na ukosefu wa ujuzi na utaalam wa jinsi ya kufuga, mitaji ya uwekezaji, uzalishaji wa chakula bora cha kuku, gharama kubwa za chakula sambamba na viwanda vinavyochakata kuku na mazao yatokanayo na kuku.

“Kumekuwa na  changamoto nyingi katika tasnia hii ya kuku  sambamba na  fursa ambazo hazijaweza kufikiwa ndio maana  SAGCOT imekuwa ikifanya kazi  kwa karibu na wabia wa maendeleo ikiwemo  T-PEC yenye  kituo cha utoaji  mafunzo ya ufugaji  wa kisasa wa kuku.

“SAGCOT inafanya kila jitihada kuhakikisha hayo mafunzo yanayotolewa chuoni hapo   yanawafikia wakulima, wafugaji na kuhakikisha yanatoa mchango stahiki katika kuwainua kiuchumi katika kongani ya Ihemi.” amesema Mgaramo.

Mgaramo amebainisha kuwa ubia mkakati wa kuku unaundwa na wabia 22 wakiwemo wafugaji wadogo wa kuku, sekta binafsi kama vile Silverlands, AKM Glitters, Tanfeed (Moragg), NMB, CRDB, Agrovets; sekta ya umma Asasi za Wanachama wa Sekta ya Kuku kama vile Tanzania Animal Feed Manufacturer Association (TAFMA), Tanzania Poultry Breeders Association, Poultry Layers Association.

Kwa mujibu wa takwimu za FAOSTAT, za mwaka 2017, Tanzania ilichakata takriban tani 104,000 za nyama ya kuku huku kiwango cha ukuaji wa jumla wa miaka 5 (CAGR) wa asilimia 4.

SAGCOT imekuwa chachu na muhamasishaji mkubwa katika kuwaunganisha wakulima wadogo, wafugaji wadogo na kuwajengea uwezo ili kuweza kutoa mchango stahiki katika sekta za kilimo mifugo na uvuvi kwa kuwafanya wadau kuingia katika kilimo biashara na kuweza kujenga uchumi himilivu na endelevu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Elimu ya utunzaji wa mazingira ipewe kipaumbele kwa watoto

Spread the love  JAMII imetakiwa kuwajengea Watoto tabia ya utunzaji wa mazingira...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

Biashara

Sloti ya Wild 81 malipo kwa njia 81 Meridianbet kasino

Spread the love Meridianbet kuna mchezo wa sloti wa kusisimua sanaambao utakufurahisha....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

error: Content is protected !!