Monday , 20 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yaainisha mpango wa kusaidia wachimbaji wadogo
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaainisha mpango wa kusaidia wachimbaji wadogo

Anthony Mavunde
Spread the love

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ameainisha mpango wa Serikali wa kusaidia utatuzi wa changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Alhamisi wakati akijibu swali la wa Viti Maalum (CCM), Dk. Christine  Ishengoma Mbunge aliyetaka kujua mpango wa Serikali kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini wilaya ya Ulanga.

Ameongeza kwamba, mpango wa Serikali ni kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini wakiwemo wachimbaji wa madini wa Wilaya ya Ulanga unahusisha masuala mbalimbali ikiwemo kuwekeza zaidi katika utafiti wa kina kugundua uwepo wa madini katika maeneo mbalimbali ili kuwaongoza vizuri wachimbaji wadogo.

“Spika maeneo mengine ni utoaji wa leseni za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo; kutoa elimu ya matumzi ya teknolojia sahihi ya uchimbaji ili kuongeza tija; huduma ya uchorongaji kwa gharama nafuu kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO),” amesema Mavunde.

Vilevile, amesema kuwa, mpango mwingine ni kuwezesha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wachimbaji; na fursa ya ukodishaji wa mitambo na vifaa chini ya usimamizi wa STAMICO.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!