Monday , 20 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the love

SERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe 3 Mei 2024, ikisema wananchi wa wilaya kadhaa zilizoko katika Pwani ya Bahari ya Hindi, waliathirika zaidi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Tathmini hiyo imetolewa leo tarehe 9 Mei 2024, bungeni jijini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, aliyetaja wilaya zilizoathirika zaidi ikiwemo Mafia, Rufiji, Kibiti, Kilwa na Mtwara.

Kwa mujibu wa ripoti ya Waziri Majaliwa, watu watano wamepoteza maisha huku saba wakijeruhiwa. Kaya zaidi ya 7,027 zenye watu 18,862 zilipoteza makazi ambapo nyumba 2,098 ziliathirika,  kati ya hizo 678 zilibomoka kabisa, 877 zikiharibika kiasi na 543 zikizingirwa na maji.

Katika wilaya ya Kilwa, vijiji 13 katika kata 11 vimeathirika na kimbunga hicho ambapo watu watatu wamepoteza maisha, kaya 178 zenye watu 941 zikipoteza makazi baada ya kuzingirwa na maji na kukwama kwa magari 126 ikiwemo ya abiria 2,534 ambao walikwama.

Manispaa ya Mtwara, Majaliwa amesema vijiji sita viliathirika ambapo nyumba zaidi ya 30 zilibomoka na kuzingirwa maji na kusababisha watu  kukosa makazi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Majaliwa amesema Hidaya kimeathiri kata saba za Kilindoni, Miburani, Kiegeaniu, Jibondo, Ndagoni, Baleni na Kirogwe, kwa kuharibu mali, miundombinu mbalimbali ikiwemo makazi ya watu, shule, afya ambapo hospitali ya wilaya imezingirwa na maji.

Miundombinu mingine iliyoathirika ni barabara ambazo zimechimbika kwa maji, nguzo za umeme kukatika na kuanguka na mmomonyoko wa udongo ulitokea katika Bandari ya Wilaya ya Mafia.

Waziri Majaliwa amesema katika Wilaya ya Rufiji, vijiji sita ikiwemo cha Ngarambe Mashariki, Ngarambe Magharibi, Chumbi A na Chumbi B, nyumba 37 zimeathirika kwa kuta zake kuanguka na kuezuliwa mapaa.

“Kutokana na athari za Kimbunga hiki katika maeneo mbalimbali hapa nchini, Serikali imechukua hatua za haraka ili kukabiliana na athari zilizojitokeza. Hatua hizo za Serikali zimeshirikisha Wizara za Kisekta, Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na wadau wote muhimu. Aidha, Kamati za Usimamizi wa Maafa katika ngazi mbalimbali zimeshirikishwa kukabiliana na maafa yaliyojitokeza,” amesema Majaliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Kiongozi Mkuu Iran amteua mrithi wa Rais Ebrahim

Spread the loveKiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei,...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

error: Content is protected !!