Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the love

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis Katimba, amepongezwa na baraza la madiwani la halmashauri hiyo, kwa kuvuka lengo la ukusanyaji mapato hadi kufikia asilimia 98, pamoja na kuboresha ustawi wa wananchi na utawala bora. Anaripoti Mwandishi Wetu, Shinyanga…(endelea).

Pongezi hizo zilitolewa katika kikao kilichofanyika siku mbili, cha robo ya tatu ya mwaka cha baraza hilo, kilichofanyika hivi karibuni wilayani Msalala, Mkoa wa Shinyanga, kwa ajili ya kujadili na kupokea taarifa ya kamati mbalimbali za halmashauri hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya madiwani, Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, Shija Joseph Luyobya, alisema wanampongeza Katimba kutokana na ubunifu wake kwenye utendaji, uliowezesha mafanikio hayo akisaidiana na watendaji wengine wa halmashauri.

Luyobya alisema ili halmashauri hiyo ifanikiwe zaidi, aliwaomba watendaji kushirikiana na mkurugenzi huyo kwa kuwa, ana malengo chanya na Msalala.

“Mwenyekiti, sisi madiwani kwa dhati kabisa tunampongeza sana mkurugenzi mtendaji wetu wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, kwa utendaji bora wake katika kuwahudumia wananchi, kutekeleza miradi ya maendeleo, kuboresha utawala bora, upatikanaji wa Hati Safi 2023/2024,” alisema Luyobya na kuongeza:

“Zaidi tunampingeza kwa kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato ambapo mpaka sasa amekusanya 98% wakiwa wamevuka lengo la serikali kabla ya Juni 30, 2024.”

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, AbdulKadir Mfilinge aliwakumbusha wafanyakazi na watendaji kuhakikisha wanaondoa dosari zote, kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani.

Mfilinge alisema kikao kilichofanyika kati ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na wakurugenzi wote nchini, Kibaha mkoani Pwani, mapema wiki hii, kimeagiza pamoja na mambo mengine, watendaji kufanya maandalizi ya uchaguzi pia kwenda kwa wananchi kusikiliza na kutatua kero zao.

“Kikao kimeagiza kufanya maandalizi ya chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, kwa kuondoa dosari zote kabla ya uchaguzi, usimamizi wa miradi, utatuzi wa kero, kutembelea miradi,ukusanyaji wa mapato sambamba na uondoaji wa migongano baina ya wenyeviti na wakurugenzi,” alisema Mfilinge.

Alisema, Mwaka wa Fedha 2024/2025 Serikali itapeleka fedha nyingi kwenye halmashauri hiyo, ili kutekeleza miradi mbalimbali katika sekta za elimu na afya,“ fedha hizo zitakapofika, ninaomba Mamlaka za Serikali za Mitaa kuzisimamia kikamilifu.”

Akizungumzia maendeleo ya Msalala, Mfilinge alimpongeza Katimba kwa kuwezesha kupata hati safi na juhudi anazofanya kufanya vikao kazi vingi ngazi za vijiji, kata na halmashauri ili kuhakikisha dhana ya utawala bora inafanikiwa.

Katika kika hicho Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya menejimenti, ufuatiliaji na ukaguzi, Ibrahim Makana, alishauri kuongeza kasi ya makusanyo ya mapato.

“Kumbukeni kutenga fedha za mafunzo mara baada ya uchaguzi kwa viongozi, shughuli zinazoandikwa ziweze kupimika na hakikisheni makusanyo ya 60% ya miradi ya maendeleo na 10% ya wanawake, vijana, walemavu na watoto zinapelekwa kama ilivyopangwa,” alisema Makana.

Aliagiza kwamba, fedha zote zinazokusanywa kupitia mfumo wa TAUSI zipelekwe benki siku hiyo hiyo zilipokusanywa, ili kuondoa mashaka  yasizokuwa na ulazima.

Baraza hilo limehitimishwa jana Jumatano, kwa wajumbe kutaka mapato kukusanywa kwa namna yoyote lakini kwa kufuata sheria.

Pia madiwani walishauri mawakala kubadilishwa mageti mara kwa mara kwa lengo la kuondoa mazoea sambamba na kufanya doria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!