Monday , 20 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio
Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Mradi wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe.
Spread the love

MRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango aliahidi kujiuzulu endapo hautakamilika hadi kufikia Juni 2024, sasa umeanza majaribio baada ya ujenzi wake kufikia asilimia 86.7. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa mradi huo uliokwama kwa zaidi ya miaka 10, imetolewa leo tarehe 9 Mei 2024, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka unaoisha, pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa 2024/25.

Waziri huyo wa maji, amesema wizara yake kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wakiwemo taasisi ya Opec Fund na Kuwait Fund, imeendelea na utekelezaji wa mradi huo na kwamba umeanza kufanya majaribio ya kutoa maji hivyo unatarajiwa kukamilika Juni 2024.

“Wizara inatekeleza mradi wa maji Same – Mwanga – Korogwe,  utakaohudumia miji ya Same na Mwanga pamoja na vijiji 38 vya wilaya za Same na Mwanga na vijiji vitano vya wilaya ya Korogwe, hadi kufikia Aprili 2024, utekelezaji wake umefikia asilimia 86.7% na kwa sasa upo kwenye majaribio ya kutoa maji kutoka chanzo na kuyapeleka kwenye chujio. Unatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu na utakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi 456,931,” amesema Aweso.

Aweso amesema mradi huo ambao ungeitia doa na kuifedhehesha wizara yake kutokana na kuonekana kuwa umeshindikana, umefanikiwa kutekelezwa kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan, kuufanya kipaumbele kwenye serikali yake.

“Nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais Samia, alivyoingia alisema kipaumbele chake cha kwanza, cha pili na tatu ni mradi wa Same – Mwanga, naomba nitoe taarifa kwa waheshimwa wabunge kuwa mradi huu ambao ulikuwa mgumu leo Dkt. Samia ameugeuza kuwa biskuti na wananchi sasa wanaenda kupata maji safi na salama,” amesema Aweso.

Tarehe 21 Machi 2024, alipotembelea mradi huo, Dk. Mpango aliiagiza Wizara ya Maji ikamilishe mradi huo ifikapo Juni mwaka huu na kwamba ikifika mwezi huo pasina kutoa maji ataacha kazi kwa kuwa viongozi hawawezi kuwaambia wananchi wasubiri huduma hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Elimu ya utunzaji wa mazingira ipewe kipaumbele kwa watoto

Spread the love  JAMII imetakiwa kuwajengea Watoto tabia ya utunzaji wa mazingira...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 85,471 walioenguliwa kipindi cha JPM wapandishwa vyeo

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 hadi sasa jumla...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

error: Content is protected !!