Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mahakama yamwekea kigingi Trump urais 2024
Kimataifa

Mahakama yamwekea kigingi Trump urais 2024

Donald Trump
Spread the love

MBIO za aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump kuliongoza tena taifa hilo, zimeingia doa baada ya kuwekewa kipingamizi cha kugombea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2024 na Mahakama ya Juu ya Jimbo la Colorado, akituhumiwa kufanya uasi akiwa madarakani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Trump aling’olewa madarakani 2020 baada ya kuangushwa katika uchaguzi mkuu, ambapo aliyekuwa mpinzani wake wa karibu, Joe Biden alishinda kiti cha urais. Kwa sasa Trump anatafuta nafasi ya kurejea kwenye wadhifa huo.

Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, uamuzi wa mahakama  uliotolewa jana Jumanne, unamzuia Trump kugombea kinyang’anyiro cha kura ya maoni kuomba ridhaa ya chama chake cha Republican, kumteua kugombea Urais wa Marekani kwenye uchaguzi ujao.

Katika uamuzi wake, mahakama hiyo imesema zuio hilo linatokana na matakwa ya kifungu cha 14 cha Katiba ya Marekani, ambacho kinazuia watu wenye kashfa za uasi kushikilia uongozi wa umma.

Aidha, mahakama hiyo imeamua kwamba, zuio hilo litadumu hadi Januari mwakani endapo Mahakama ya Juu ya Marekani, itatoa uamuzi dhidi ya mashtaka mbalimbali yanayomkabili Trump. Kama Trump ataonekana hana hatia katika mashtaka hayo, zuio hilo litabatilishwa na kama atakutwa na hatia litaendelea kufanya kazi.

Mahakama hiyo imetoa maoni yake kwamba, kwa kuwa mchakato wa kura za kuchuja wagombea katika Jimbo la Colorado ni tarehe 5 Januari 2024, Chama cha Repubilican kiteue mgombea mwingine tofauti na Trump, atakayechuana na mgombea urais mtarajiwa wa chama cha Democratic, Joe Biden, ambaye anamaliza muda wake.

Hata hivyo, uamuzi huo umetajwa kutoathiri kwenye majimbo mengine ingawa tayari umemtia dosari Trump, kwa kuwa hatoweza kugombea katika jimbo hilo, kama zuio hilo halitabatilishwa.

Miongoni mwa sababu za mahakama ya Colorado kumwekea zuio Trump kugombea, ni tuhuma zinazomkabili za wafuasi wake kufanya uasi kwenye Ikulu ya Marekani tarehe 6 Januari 2021, ambapo walifanya vurugu wakipinga ushindi wa Rais Biden, kwenye chaguzi uliofanyika 2020.

Si Colorado pekee, Trump anatajwa kuandamwa na vizuizi vya kugombea katika uchaguzi huo ambapo mahakama kadhaa za Marekani zinaendesha mashauri mbalimbali yanayolenga kumwekea zuio la kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho, wakidai anakabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo ya uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya madaraka.

Wafuasi wa Trump wamepinga uamuzi huo wakidai sio wa kidemokrasia, huku wakiweka matarajio juu ya Mahakama ya Juu ya Marekani, kwamba itatoa uamuzi wa kubatilisha zuio hilo.

Mahakama za majimbo ya Minnesota, Michigani, Rhode Island na Florida,  zilitupilia mbali mashtaka hayo zikisema hazina mamlaka ya kumzuia mtu kugombea katika kura za awali za maoni ndani ya chama chake, huku sababu nyingine ikitajwa kuwa wafunguaji wa maombi hayo hawakuwa na nguvu kisheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!