Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari Kubenea ambwaga Makonda kesi ya ‘mchongo’
HabariTangulizi

Kubenea ambwaga Makonda kesi ya ‘mchongo’

Saed Kubenea
Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imefuta hukumu iliyomtia hatiani aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo (2015-2020), Saed Kubenea na kupewa adhabu ya kukaa miezi mitatu bila kufanya kosa lolote. Anaandika Faki Sosi Ubwa…(endelea).

Itakumbukwa kuwa tarehe 13 Aprili, 2016, aliyekuwa Hakimu Mkazi Thomas Simba, alimtia Kubenea hatiani kwa makosa ya kumtolea maneno ya kumtusi na kumkashifu Paul Makonda wakati huo akiwa Mkuu wa Wilaya Kinonndoni.

Uamuzi wa kufuta hukumu hiyo umetolewa mahakamni hapo jana tarehe 17 Agosti, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu Romuli Mbuya baada ya kupitia upya mwenendo wa kesi hiyo kama ilivyoamriwa na Mahakama Kuu kufuatia rufaa ya Kubenea kupinga hukumu hiyo.

Paul Makonda

Katika hukumu yake Hakimu Mbuya amesema kuwa kuna tofati mkubwa wa maneno, kati ya hati ya mashtaka, mlalamikaji, Makonda, shahidi wa pili PC Gabriel na shahidi wa tatu aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Polisi ya Magomeni, ASP Denis Mujumba.

“Tofauti hiyo ya maneno inatosha kusema kuwa Jamhuri imeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya Kubenea,” amesema Hakimu Mbuya.

Aidha ameweka wazi kuwa upande wa Jamhuri ulikuwa na mashahidi wenye maslahi ya kulinda vibaria vyao kwa kuwa wakati huo Makonda alikuwa bosi wao, “mashahidi hao hawakuwa watu huru kuweza kutoa ushahidi utakaokinzana na Bosi wao.”

Kubenea alishtakiwa kwa kudaiwa kumtukana Paul Makonda akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, ambapo tarehe 15 Desemba 2015 wawili hao walikutana eneo la miwanda cha Tooku Garments Co. Limited.

Kubenea alifika hapo kusikiliza kero za wafanyakazi wa kiwanda hicho ambapo naye Makonda alifika na kumzuia asizungumze na wafanyakazi hao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

error: Content is protected !!