Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NCT kutoa mafunzo ya utalii kwa wadau 5,000
Habari Mchanganyiko

NCT kutoa mafunzo ya utalii kwa wadau 5,000

Spread the love

CHUO Cha Taifa Cha Utalii (NCT), kimejipanga kutoa mafunzo kwa wadau waliokwenye mnyororo wa utalii yatakayowezesha nchi kufikia malengo ya kuingiza watalii milioni 5 kwa mwaka hadi kufikia mwaka 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Afisa Mtendaji Mkuu, Dk. Shogo Mlozi aliyasema hayo jana, jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo yao ambayo yatazinduliwa leo (jumamosi).

Afisa Mtendaji Mkiuu Chuo cha Taifa cha Utalii, Dk. Shogo Mlozi akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi kuhusu uimarishaji huduma-mafunzo kwa wadau walio katika Mnyororo wa huduma za utalii

Alitaja baadhi ya taasisi ambazo zimelengwa kupewa mafunzo hayo kuwa ni maafisa uhamiaji, maafisa Polisi, waendeshaji wa vyombo vya usafiri, wauzaji wa vyakula mbalimbali, watu maarufu, waandishi wa habari na wadau wengine muhimu.

Dk. Mlozi alibainisha kwamba kupitia mpango huo, chuo kimekusudia kuwafikia wadau zaidi ya 5,000 kutoka Dar es salaam, Zanzibar, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Mara na mikoa mingine ya Tanzania.

“Chuo kimeazimia kuanza mafunzo katika mikoa hii Kwa kuzingatia kuwa mikoa hii ni maeneo yaliyo na huduma nyingi za kitalii, lakini pia ndio maeneo makuu Kwa watalii kuingia na kutoka nchini.” Alisema Dk. Mlozi.

Akizungumzia kuhusu mpango huo amesema, awali wataanza kutoa mafunzo kwa maafisa uhamiaji wapatao 700.

Anasema sababu kubwa ya kuanza na maofisa uhamiaji inachangiwa na wao kukutana na wageni wengi wenye mahitaji mbalimbali wanaotoka au kuingia nchini Kwa shughuli tofauti ikiwemo ya utalii.

“Ili kufikia malengo ya kuongeza watalii nchini ni lazima kujenga mahusiano mazuri baina ya sekta ambazo kwa njia moja huchangia maendeleo ya sekta ya utalii. hivyo shughuli za ulinzi za ulinzi na usalama ni eneo muhimu sana kwa ustawi wa sekta ya utalii,” alisema Dk. Mlozi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Dk. Shogo Mlozi akizungumza na Meneja Mwandamizi wa Benki ya NMB, Theresia Mayanie (kulia) wakati wa Mkutano na waandishi kuhusu uimarishaji huduma-mafunzo kwa wadau walio katika Mnyororo wa huduma za utalii, Kushoto ni Msemaji wa Jeshi la Uhamiaji Paul Mselle

Akizungumzia kuhusu lengo jingine la mafunzo hayo alisema ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuinua sekta ya utalii na kuwa stahimilivu zaidi baada ya kudorora Kwa huduma kutokana na janga la UVIKO-19.

“Tumejipanga kuunga mkono jitihada za Rais Samia kupitia programu ya Royal Tour katika kufikia malengo ya kufikisha watalii milioni Tano kwa mwaka ifikapo mwaka 2025.” Alisema

Anasema kuwa Rais Samia kwa kupitia Royal Tour kwao wanapona kama ni pasi ya kuleta watalii ili wadau wawachangamkie kama fursa.

Aliongeza kuwa baadhi ya mada zitakazofundishwa ni Wageni naumuhimu wao, sifa zamtoa huduma, Matumizi na usimamizi wa muda, Uwezo wa kuwasiliana, utoaji wa huduma Bora kwa wateja, kushughulikia malalamiko ya wateja, kumsaidia mteja mwenye mahitaji maalum, usalama wa mali za wageni pamoja na bidhaa na huduma za kitalii zilizopo nchini.

Katika uzinduzi huo unaotarajia kufanyika Agosti 20, 2022, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Pindi Chana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!