Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari Kipa Yanga aibukia Rwanda  
HabariMichezo

Kipa Yanga aibukia Rwanda  

Ramadhani Awam Kabwili of TanzaniaTanzania players during the 2017 Under 17 Africa Cup of Nations Finals football Tanzania training session at the Libreville Stadium in Gabon on 17 May 2017 ©Samuel Shivambu/BackpagePix
Spread the love

 

Aliyekuwa mlinda mlango wa klabu ya Yanga Ramadhan Kabwili, rasmi amejiunga na klabu ya soka ya Rayon Sport ya nchini Rwanda kama mchezaji huru mara baada ya kumalizika kwa mkataba na klabu yake ya zamani ya Yanga. Anaripoti Damas Ndelema………(endelea)

Mchezaji huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuweza kuitumikia klabu hiyo, inayoshiriki Ligi Kuu nchini Rwanda ambyao wanapambana kutengeneza timu yao ili kurejesha ufalme wao katika soka la nchini humo baada ya msimu uliopita kushika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu nchini humo.

Kipa huyo alieibukia katika michuano ya Afcon 2017 akionesha kiwango bora akiwa na timu ya Taifa ya vijana kisha kujiunga na timu ya Yanga ambpo alipewa kandarasi ya miaka mitano.

Kabwili amesajiliwa kwenye klabu bhiyo kwa mapendekezo ya kocha wa makipa wa timu hiyo, Vladimir Niyonkuru raia wa Burundi ambae pia aliwahi kufanya nae kazi wakiwa wote kwenye klabu ya Yanga, chini ya kocha Mwinyi Zahera raia wa Congo.

Mlinda mlango huyop alithibitisha rasmi kijiunga na miamba hiyo ya nchini Rwanda, kupitia kurasa yake inayopatikana kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram na kuandika kuwa ni muda wa kufungua ukurasa mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

Michezo

Anza Jumamosi yako na mkwanja wa Meridianbet

Spread the loveJumamosi ya leo ODDS zimekaa kijanja sana ndani ya Meridianbet...

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

error: Content is protected !!