Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Adama Barrow atangazwa mshindi uchaguzi Gambia
Kimataifa

Adama Barrow atangazwa mshindi uchaguzi Gambia

Spread the love

 

Rais wa Gambia, Adama Barrow ameshinda tena uchaguzi mkuu wa nchi hiyo katika kura zilizopigwa kwa mara ya kwanza kwa miongo kadhaa bila ya kiongozi wa muda mrefu Yahya Jammeh. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Rais Barrow amepata takriban asilimia 53 ya kura za Jumamosi, huku mpinzani wake wa karibu – wakili, Ousainou Darboe – akiwa na kura asilimia 28.

Darboe na wagombea wengine awali walisema hawakubaliani na matokeo ya uchaguzi huo.

Kura hizo zinaonekana kama jaribio la demokrasia nchini humo.

Katika uchaguzi uliopita, Barrow alimshinda Yahya Jammeh, ambaye sasa anaishi uhamishoni baada ya kukataa kukubali matokeo.

Utawala wa miaka 22 wa Jammeh ulighubikwa na madai ya unyanyasaji, na mashahidi hivi karibuni waliiambia tume ya kuhusu wahusika wa utekelezaji wanavyoungwa mkono na serikali.

Licha ya uhamisho wake, Jammeh bado ni mtu mwenye ushawishi mkubwa, alifanya kampeni akiwa mbali na kuwataka na kuwataka wananchi kutompigia kura Barrow.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!