Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Elsie Kanza amekutana kwa mazungumzo na Meya wa mji wa Dallas, Meya Eric Johsnon pamoja na kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Watanzania (Diaspora) waishio Marekani na Mexico. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)
Mazungumzo kati ya Balozi Kanza na Meya Eric Johnson yalilenga katika kuimarisha uchumi wa kidiplomasia hususan katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji.
Balozi huyo amemuomba Meya Eric kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji kuja Tanzania kuwekeza kutokana na uwepo wa fursa nyingi huku mazingira ya biashara na uwekezaji yakiwa yameboreshwa kwa kuondoa kodi kero tangu serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan uingie madarakani.
Katika mkutano na Watanzania waishio Marekani na Mexico amezungumzia juu ya namna ya kutangaza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zilizopo Tanzania pamoja na kuweka mikakati ya kuwavutia watalii wengi kwenda Tanzania kutembelea vivutio mbalimbali vya uwekezaji.
Pia Balozi Kanza amefanya mazungumzo na Watanzania (diaspora) waishio Marekani katika Majiji ya Texas na Houston kwa lengo la kujitambulisha katika jumuiya hiyo na kujadiliana masuala mtambuka kuhusu maendeleo ya Tanzania.
Leave a comment