Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari Wakazi Ukerewe, Mbinga waibuka washindi NMB Bonge la Mpango
Habari

Wakazi Ukerewe, Mbinga waibuka washindi NMB Bonge la Mpango

Spread the love

 

DROO ya nane ya Kampeni ya ‘NMB Bonge la Mpango – 2merudi Tena,’ imefanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha, ambako Theofrida Masudi wa Nansio Ukerewe, mkoani Mwanza na Haikamesia Mcharo wa Mbinga, Mkoa wa Ruvuma waliibuka washindi wa pikipiki za miguu mitatu ainanya Skymark. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Bonge la Mpango ni kampeni ya miezi mitatu inayoendeshwa na Benki ya NMB, ikilenga kuhamasisha utamaduni chanya wa kuweka akiba, ambako kila wiki washindi 12 hupatikana, 10 kati yao huzawadiwa fedha taslimu huku wawili waliibuka na Skymark zenye thamani ya Sh.4.5 milioni kila moja.

Katika droo hiyi iliyofanyika Ofisi za NMB Tawi la Clock Tower, chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), ilishuhudiwa wateja wa mikoani wakiendelea kutikisa kampeni hiyo kwa kuibuka na zawadi kubwa za Skymark kwa wiki ya nne mfululizo, tangu mshindi wa Dar es Salaam alipopatikana kwenye droo ya nne.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Dismas Prosper, alisema washindi hao 12 waliopatikana katika droo hiyo, ni mfululizo wa wateja walionufaika na kampeni hiyo, ambayo itafikia ukomo mwishoni mwa mwezi huu wa Desemba.

Dismas aliwataka wateja wa NMB kuendelea kujiwekea akiba ili kushinda zawadi mbalimbali, huku akitoa wito kwa wasio na akaunti NMB, kufungua na kuweka akiba isiyopungua Sh. 100,000 ili kukidhi vigezo vya ushiriki wa droo hiyo na kujishindia zawadi za pesa taslimu na pikipiki za Skymark.

Ukiondoa Theofrida na Haikamesia waliojishindia Skymark, washindi wa pesa taslimu waliopatikana katika droo hiyo ya nane (na matawi yao kwenye mabano) ni pamoja na Calvalina Stephani (Magomeni), Adeodatha Raphael (Mpanda) na Saidi Ligongo (Kibiti).

Wengine ni Floriana Mcharo (Mwenge), Deus Masai (Sengerema), Gaundence Mwakitaku (Nelson Mandela), Essay Kapia (Kambarage), Morin Msukwa (Mbozi), Faruki Bakari (Namanga) na Faraja Kusasula (Temeke).

Aidha, Meneja Mahusiano Amana za Wateja wa NMB, Monica Job, amesema washindi 12 waliopatikana katika droo ya nane, wanafanya idadi ya wanufaika wa Bonge la Mpango kufikia 99, Kati yao 80 wakijinyakulia pesa taslimu na 19 wakibeba pikipiki za Skymark.

“Kufikia sasa tumetoa jumla ya washindi 99, Kati ya hao, 80 wameshinda pesa taslimu Sh.8 milioni huku washindi 19 wakitwaa pikipiki (19), mbili za kila wiki na tatu za mwisho wa mwezi, zote kwa ujumla zikiwa na thamani ya Sh93.5 milioni.”

“Tunawapongeza washindi wote, huku tukiwahimiza wengine kuendelea kujiwekea akiba ili kujiongezea nafasi za kushinda zawadi mbalimbali katika mwezi huu wa mwisho wa kampeni hii,” alisema Monica.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!