JESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad Slaa na Wakili Boniface Mwabukusi kufuatia kufanya mkutano wa hadahara ambao ulikuwa unadaiwa kwamba haukuwa na kibali, Anaripoi Kelvin Mwaipungu …(endelea)
Wito huo wa jeshi hilo ulitolewa jana, Oktoba 8, 2023 kwa njia ya barua mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo ambao ulifanyika kwenye kijiji cha Kandete, Halmashauri ya Busekelo.
Katika barua hiyo iliyotoka kwenye ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, iliwataka wawili hao kufika hii leo kwenye kituo Kikuu cha Polisi Mbeya majira ya saa 8, mchana kwa ajili ya mahojiano, kama sehemu ya upelelezi kwenye kesi hiyo.
Jana Video zilionesha Mwabukusi akiwa juu ya jukwaa akiwatangazia wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo kuwa Polisi wamefika viwanjani hapo kuzuia mkutano huo kwa sababu palipigwa nyimbo za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kwamba wenyewe wamelalamika kwa jeshi la Polisi.
“Polisi wanasema kuwa wamezuia kusanyiko hili eti kisa kumepigwa wimbo wa chadema hivyo wanataja tukakate rufaa kwa Waziri husika” alisikika Mwabukusi kwenye kipaza video hiyo
Endelea kutembelea MwanaHALISI Online kwa ajili ya kukujuza nini kinachoendelea
Leave a comment