Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Watu 1,000 wafariki vita Israel, Palestina
KimataifaTangulizi

Watu 1,000 wafariki vita Israel, Palestina

Spread the love

 

MAPIGANO ya kijeshi kati ya Kundi la Hamas la Palestina na Jeshi la Israel, yaliyoanza Jumamosi iliyopita, yamepoteza maisha ya watu zaidi ya 1,000, huku maelfu wakijeruhiwa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Mitandao hiyo imeripoti kuwa, Waisrael 700 wameuawa huku 100 wakitekwa na wanajeshi wa kundi la Hamas, huku kwa upande wa Palestina, raia wake 400 wamefariki dunia, kufuatia mashambulizi ya anga.

Wakati vita hiyo ikizidi kushika kasi, Rais wa Marekani, Joe Biden ameahidi kuwa Serikali yake itatoa misaada ya kijeshi kwa Israel, ili kuiongezea nguvu katika kukabiliana na Palestine, akidai kwamba uamuzi wa taifa hilo la kiislamu kuanzisha mashambulizi mfulkulizo upande wa Israel.

Serikali ya Marekani imeahidi kupeleka shehena za ndege na meli za kijeshi , pamoja na silaha nyingine nzito nchini Israel .

Mbali na Serikali ya Marekani ikitangaza kuisaidia Israel, Rais wa Iran, Ebrahim Raisi, ameahidi kuisadia Hamas, ambapo hadi sasa taifa hilo linadaiwa kukisaidia kikundi hicho kwa kukipatia roketi, ndege zisizo na rubani na wanamgambo.

Hamas ilianzisha mashambulizi kusini mwa Israel, kitendo kilichopelekea taifa hilo kujibu mashambulizi kwa kushambulia eneo lake la Ukanda wa Gaza.

Kufuatia mapigano hayo, mitandao ya kimataifa imeripoti wapalestina zaidi ya 120,000 wameyakimbia makazi yao.

Mtandao wa Aljazeera umeripoti kuwa, mapigano ya bunduki yanaendelea kwa siku ya tatu mfululizo kati ya wapiganaji wa Hamas na vikosi vya Israel, kwenye maeneo makuu matatu ya Israel.

Kufuatia machafuko hayo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN), lilikutana kwa dharura ili kujadili mzozo huo lakini lilishindwa kupata muafaka wa kuyasitisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataka jamii inayohoji mafisadi

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo juu ya uboreshaji dira...

Habari za SiasaTangulizi

Kapinga: Kukatika kwa umeme siyo hujuma

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali ipo kazini...

error: Content is protected !!