Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi
ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the love

NAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)  kwa kutoa mafunzo ambayo yanaendana na soko la ajira na kuwashauri wawe na utaratibu wa kuwatafutia ajira wanafunzi wa chuo hicho  kabla hawajamaliza elimu yao chuoni hapo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Aliyasema hayo leo  wakati akizungumza kwenye hafla ya kutiliana saini baina ya Wakala wa Vipimo (WMA) na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), kuhusu mafunzo ya uanagenzi kwa wanafunzi.

Alisema wenye kampuni kubwa nchini hasa za mitandao ya simu wanawataalamu wa hali ya juu ambao ni watanzania na wamekuwa wakiwapata kwa kutembelea vyuoni kuangalia wenye vipaji.

“Mafunzo mnayotoa ni ya hali ya juu kwa hiyo hakuna sababu mwanafunzi akamaliza masomo yake hapa akakosa ajira  na ninawapongea kwa ushirikiano ambao mmeuanzisha na WMA kwasababu nafahamu utanufaisha pande zote mbili,” alisema Zungu

Zungu pia alikitaka chuo cha CBE kuendelea kujitangaza ndani na nje ya nchi ili kiweze kupata wanafunzi kutoka nchi za kigeni kama ilivyo kwa vyuo vingine kama Chuo cha Afya Muhimbili MUHAS na Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), ambayo inapata wagonjwa wengi wa nje ya nchi.

Naibu Spika, Musa Azzan Zungu akizungumza wakati wa utilianaji saini wa kutoa mafunzo ya uanagenzi (mafunzo kwa vitendo) baina ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Wakala wa Vipimo (WMA), hafla iliyofanyika leo chuoni hapo.

“Hiki chuo nakifahamu miaka mingi sana mko mahiri sana katika kutengeneza wataalamu lakini lazima muongeze nguvu kwenye kitengo chenu cha masoko jitangazeni usiku na mchana dunia ijue kazi mnayofanya na mtapata wanafunzi wengi sana ndani na nje ya nchi,” alisema Zungu

Mkuu wa Chuo cha CBE, Profesa Edda Lwoga, alisema kupitia mafunzo ya uanagenzi, wanafunzi wa Shahada ya kwanza ambao wanasoma miaka mitatu watasoma mwaka mmoja na nanusu shuleni na mwaka mmoja na nusu kazini ili wapate elimu ya vitendo itakayowasababisha wawe mahiri kazini.

“Kupitia huu mkataba mwanafunzi wa CBE anayesomea kozi ya vipimo atakuwa anasoma muhula wa kwanza chuoni na muhula wapili anakwenda kufanyakazi WMA ilia pate elimu kwa vitendo na hii kozi ya vipimo inafundishwa na chuo hiki pekee na Afria Mashariki na Kati ni sisi tu tunaotoa kozi hii,” alisema

.Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Edda Lwoga (kulia), akibadilishana nyaraka baada ya kusaini makubaliano ya kutoa mafunzo ya uanagenzi, kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA), Stella Kahwa.

Alisema ili kuendesha kozi hiyo ya vipimo  kwa umahiri lazima washirikiane na waajiri na kwamba tayari CBE ilishasaini makubaliano na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili wapate wahitimu ambao wanakubalika sokoni.

Alisema kozi hiyo itatolewa na CBE kuanzia ngazi ya Cheti, Stashahada na Shahada  na mwaka huu wa fedha chuo kimeshapata vitendea kazi vya kozi hiyo ambavyo ni mafuta ya petroli, dizeni na mafuta ya ndege na mafuta ya taa vyenye thamani ya milioni 200.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa (WMA), Stela Kahwa, alisema wakala ulikuwa unasubiri siku ya kusaini makubaliano hayo kwa hamu kwani wanamatumaini makubwa ya kunufaika na ushirkiano huo kwa kupata wataalamu bobezi wengi kwenye fani ya vipimo.

Mgeni rasmi Naibu Spika, Musa Azzan Zungu akiwa kwenye picha ya pamoja na walioshiriki kwenye hafla ya kusaini makubaliano baina ya Chuo cha Elimu ya Biashara CBE na Wakala wa Vipimo WMA.

Alisema CBE kwa muda mrefu imekuwa ikitoa wataalamu ambao wamekuwa msaada mkubwa kwa WMA na kusema kuwa hata yeye ni matunda ya chuo hicho kwani alihitimu mwaka 1985.

Alisema kazi ya wakala ni kuhakiki vipimo kuhakikisha vinakuwa sawa na hakuna mwananchi anayepunjwa akisisitiza kuwa kwa kuwa teknolojia inabadilika kwa kasi basi na mitaala ya vipimo nayo inapaswa kubadilika mara kwa mara kwenda na wakati.

“Kama hufanyi maboresho ya mitaala unaweza kukuta yule ofisa vipimo uliyemfundisha anakuja kwenye soko la ajira vile vipimo ulivyomfundisha havipo kwa sababu hata mimi vipimo vingi nilivyojifunza mwaka 1985 sasa hivi havipo kwa hiyo tusipoboresha mitaala tutapitwa na wakati,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

error: Content is protected !!