Monday , 6 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mwanaume afunga ‘ndoa’ na rice cooker
Kimataifa

Mwanaume afunga ‘ndoa’ na rice cooker

Spread the love

 

UKISTAAJABU ya Mussa uyataona ya Firauni. Ndivyo unavyoweza kuelezea kile alichokifanya Khoirul Anam, raia wa Indonesia aliyeamua kufunga ‘ndoa’ na ‘rice cooker.’ Anaripoti Mitanga Hunda, TUDARCo … (endelea).

Unaweza fikiria ni simulizi, lahasha ni kweli mwanaume huyo ameamua kufunga pingu za maisha na kifaa hicho cha kupikia na picha zake kuibua mjadaa.

Picha ndoa hizo, amezeweka wiki mbili zilizopika katika ukurasa wake wa facebook na kuibua mjadala wa namna gani hicho alichokifanya kinashangaza.

Yeye pamoja na ‘mke wake’ huyo ambaye ni rice cooker walivalia mavazi meupe na akionekana kuibusha rice cooker hiyo ambayo ilifunikwa kwa shera mithili ya bibi harusi.

Picha hizo alizoweka kwenye facebook, zilikwenda sambamba na maneno akisema, nyeupe, nyeupe, nyeupe, mwenye upendo. Sina maneno mengi ya kusema. Mimi ni mahiri wa kupika.

Bila wewe mchele wangu siwezi kuupika. Akaweka emoji za kucheka na kumalizia akisema burudani.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!