MWENDESHA mashitaka nchini Ujerumani, ameanza uchunguzi dhidi ya raia mmoja wa Uturuki, anayetuhumiwa kwa ujasusi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Ofisi ya mwendesha mashitaka mkuu nchini humo imesema, inamchunguza mtu aliyekamatwa wiki mbili zilizopita kwa madai ya kufanya ujasusi kwa niaba ya idara ya kijasusi ya Uturuki.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika mji wa Dusseldorf.
Msemaji wa mamlaka hiyo yenye makao yake mjini Karlsruhe, ameliambia shirika la habari la Ujerumani (DPA), kulikuwa na ushahidi wa kutosha unaoshiria mtu huyo alikusanya taarifa kuhusiana na wafuasi wa kile kinachoitwa vuguvugu la Gulen katika eneo la Köln.
Uturuki inamlaumu kiongozi wa kidini anayeishi Marekani, Fethullah Gulen kwa kuandaa jaribio la mapinduzi la 15 Julai 2016, lililoshindwa.
Mamlaka za Ujerumani zilimkamata mtu huyo tarehe 27 Septemba katika operesheni pana ya kipolisi na baadaye idara ya masuala ya dharura ziling’amua nyaraka zilizoashiria kitisho kwa baadhi ya watu.
Leave a comment