October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kagere arejesha furaha msimbazi

Spread the love

BAO pekee lililofungwa dakika ya 69 na mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagera dhidi ya Dodoma Jiji limerejesha furaha kwa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara. Anaripoti Damas Ndembela,TUDARCo…(endelea).

Simba imeibuka na ushindi huo leo Ijumaa, tarehe 1 Oktoba 2021 katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

Kagere ambaye ni raia wa Rwanda, alifunga bao hilo akiunganisha pasi safi ya mshambuliaji mwenzake, Chris Mugalu.

Ni ushindi wa kwanza kwa Simba wa msimu mpya wa ligi kuu 2021/22. Wiki iliyopita Simba ilitoka sare katika mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya BiasharaUnited.

Mara baada ya mchezo huo, kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema “mechi ilikuwa ngumu na naweza kusema ilikuwa kama vita. Tunawapongeza wachezaji kwa kujituma kikubwa tumepata alaatatu muhimu.”

Ushindi huo kwa Simba ni wa kwanza katika michezo minne iliyocheza ikiwemo ya kirafiki na ngao ya jamii.

Ilifungwa katika kilele cha Simba Day 1-0 dhidi ya TP Mazembe kisha ikakubali kipigo kama hicho cha 1-0 kutoka kwa watani zao Yanga kwenye Ngao ya Jamii. Kisha ikatoka sare na Biashara United.

error: Content is protected !!