Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe apenyeza ujumbe Ikulu
Habari za SiasaTangulizi

Membe apenyeza ujumbe Ikulu

Spread the love

NCHI haiwezi kustawi bila ya uhuru wa vyombo vya habari. Kukosekana kwa uhuru huo, kunadumaza maendeleo ya nchi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Huo ni ujumbe wa Bernard Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali ya awamu ya nne iliyoongozwa kwa miaka 10 na Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza wakati akitoa salamu katika shughuli ya kuuaga mwili wa mwanahabari, Godfrey Dilunga katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo tarehe 19 Septemba 2019, Membe amesema ustawi wa uhuru ndio ustawi wa nchi.

Amesema, taifa ili listawi, halina budi kuhakikisha kunakuwepo na uhuru wa vyombo vya habari, na kwamba uhuru huo ni sawa na mbolea katika ustawi wa taifa, kinyume chake nchi inakuwa dumavu.

“Kifo hiki kitukumbushe kitu kimoja, kitukumbushe uhuru wa vyombo vya habari kwamba ni sawa na mbolea inayowekwa kwenye mche ili uchipue vizuri na kuzaa matunda.

“Bila ya vyombo vya habari, nchi inakuwa dumavu. Afya ya serikali yoyote duniani inatokana na vyombo vya habari,” amesema Membe.

Kiongozi huyo wa serikali iliyopita, ametoa kauli hiyo huku kukiwa na malalamiko yanayoelekezwa katika serikali ya sasa, inayoongozwa na Rais John Magufuli kwamba inaminya uhuru wa vyombo vya habari.

Aidha, Membe amewataka wanahabari kuiga mfano mwema wa Dilunga, aliyekuwa mwandishi mwenye maadili anayesimamia ukweli, misimamo na haki katika uandishi enzi za uhai wake.

“Tuige mfano wake, tuwe huru, tuseme kweli ili nchi ifike inakostahili bila woga,” amehimiza Membe.

Dilunga ambaye alikuwa Mhariri wa gazeti la wiki la Jamhuri, amefariki dunia alfajiri ya tarehe 17 Septemba 2019, wakati akipatiwa matibabu ya maradhi ya tumbo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Wanaotaka kujifunza ZEC kwao kukoje?

Spread the loveMKURUGENZI wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Thabit Idarous...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Biteko, Nape wanadanganya?

Spread the loveKWA mila na desturi zetu za Kiafrika mkubwa huwa hakosei,...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miamka 60 ya Muungano: Tunakwama wapi?

Spread the loveRAIS wa Jamhuri, Samia Suluhu Hasssan, Ijumaa iliyopita, aliongoza mamilioni...

error: Content is protected !!