October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kumwaga Dilunga: Polepole asema ‘nampenda Zitto’

Spread the love

HUMPHREY Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema, anampenda Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Polepole ametoa kauli hiyo leo tarehe 19 Septemba 2019, katika shughuli ya kuuaga mwili wa mwanahabari, Godfrey Dilunga iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Dilunga ambaye mpaka mauti yanamfika jana tarehe 17 Septemba 2019 jijini Dar es Salaam, alikuwa Mhariri wa Gazeti la Jamhuri akitokea Raia Mwema.

Shughuli ya kuaga mwili wake kwenye viwanja hivyo imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa na wanaharakati.

Kwenye shughuli hiyo, Polepole ametoa kauli hiyo baada ya mwanahabari Ezekiel Kamwaga, kuwataka walioshiriki kuelezana kwamba wanapendana.

“Ezekiel amesema taarifa mbayo hata mie ningependa kuiweka wazi, kati ya watu ambao chama cha mapinduzi kilimthamini ni Dilunga. Inawezekana alivyotuelekeza tuwaambie jirani yetu unampenda mi nikamwambia Zitto nampenda,” amesema.

error: Content is protected !!