Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polepole ‘apagawa’ uchaguzi Kinondoni, Siha
Habari za SiasaTangulizi

Polepole ‘apagawa’ uchaguzi Kinondoni, Siha

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM. Picha ndogo Salum Mwalimu, Mgombea Ubunge, Kinondoni akiwa katika moja ya kampeni zake
Spread the love

KIWEWE kimetawala ndani ya Chama Cha Mapinduzi baada ya wapinzani wao wakuu kwenye uchaguzi unaotarajia kufanyika Februari 17 kuapa kulinda kura kwa gharama yoyote. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ndicho kinachoipelekea puta (CCM) kwenye Uchaguzi huo ambacho kilijiapiza kulinda kura za wagombea wake baada ya kupiga kura.

Leo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amelitaka jeshi la polisi kuhakikisha Chadema hakilindi kura kwani hilo si jukumu lao.

Polepole amesema hayo leo Februari 15, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mdogo wa Ubunge na nafasi za udiwani ambao unatarajia kufanyika Februari 17 2018 na kudai kuwa mpaka sasa wamepata taarifa kuwa (Chadema) wanachukua watu kutoka mikoani kuja kulinda kura kitu ambacho hakikubaliki.

“Zipo nyumba kadhaa hapa Dar es Salaam ambazo zimehifadhi watu wasio wakazi wametoka mikoa mbalimbali kuja hapa kwa kigezo cha kulinda kura, sisi hatufanyi siasa za matukio wala kutafuta kiki baada ya kujua hili tumewajulisha jeshi la polisi juu ya nyumba hizo na watu hao, kitakachofuata ni kushugulika na watu hao ambao hawapendi utaratibu mzuri na desturi yetu nzuri ya uchaguzi” amesema Polepole.

Polepole amesema kuwa pamoja na kuwa (CCM) ndio chama kinachoongoza nchi kinalitaka jeshi la polisi kutimiza majukumu yao ya kudhiti vurugu na kwamba sio kazi ya wafuasi wa chadema kulinda kura.

“Kura hazilindwi na watu wanaoletwa kwa makundi bali kura kwa mujibu wa Katiba, Sheria ya uchaguzi na kanuni mbalimbali za uchaguzi zimewekewa utaratibu wa kisheria kuhakikisha mwenye yake na anaipata hiyo, upo utaratibu wa mawakala kila chama kina wakala huyo ndiye atakayeshiriki kuhesabu, kujua hii kura yangu au si yangu sasa unapoanza kuandaa watu wasiojulikana na kuwaleta Dar es Salaam ni kuleta taharuki na mpango huo msingi wake ni kutisha wakina mama, vijana na wazee wasijitokeze kwenda kupiga kura,

“ Tumesema jeshi la polisi tafadhali tena tafadhali sana watu wasiohusika na usimamizi wa zoezi la uchaguzi ni sheria hawapaswi kuwepo wanatakiwa kuwepo kwenye maeneo yao wakafanye kazi zao za kujiletea kipato, uchaguzi haulindwi na mabaunsa, kura hailindwi bali dola ina vyombo vyake ambavyo sisi wote vyama vya siasa tumekubaliana” alisisitiza Polepole

Wakati huo huo Polepole ameeleza namna chama hicho kilivyojipanga kushgerhrkra ushindi wa uchaguzi huo.

“Kwa namba hii CCM itakuwa na ushindi mkubwa na wa kishindo na hii tutakuwa tunatesti mitambo kwa uchaguzi mkuu 2020 na ule wa serikali za mitaa.”

Amesema kuwa chama hicho kinauhakika kitashinda uchaguzi huo majimbo yote mawili na kata zote.

“Wagombea hawa 12, wawili wa majimbo na 10 wa Kata. Kinondoni – Maulid Mtulia na Dk Godwin Mollel kule Siha na madiwani ni makini kwelikweli ambao watashughulika na matatizo ya wananchi na hawa ndio wataibuka washindi.”

Amesema kuwa wajiandae kushindwa na kuyapokea matokeo kutokana na kushindwa kutokana na hesabu za kisiasa za chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Wanaotaka kujifunza ZEC kwao kukoje?

Spread the loveMKURUGENZI wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Thabit Idarous...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Biteko, Nape wanadanganya?

Spread the loveKWA mila na desturi zetu za Kiafrika mkubwa huwa hakosei,...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Miamka 60 ya Muungano: Tunakwama wapi?

Spread the loveRAIS wa Jamhuri, Samia Suluhu Hasssan, Ijumaa iliyopita, aliongoza mamilioni...

error: Content is protected !!