March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

DPP amwachia huru Sadifa

Aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM, Sadifa Hamis

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dodoma imemwachia huru aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM, Sadifa Hamis baada ya Jamhuri kuwasilisha ombi la kuifuta kesi ya rushwa. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Sadifa ambaye ni mbunge wa Donge Zanzibar ameachiwa huru baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) kuamua kutoendelea na kesi hiyo.

Kifungu kinachompa mamlaka DPP kuamua kutoendelea na kesi yoyote ni 91(1) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai bila kuhojiwa na mamlaka yoyote.

Sadifa alituhumiwa kwa tuhuma za rushwa ya kuwataka wanachama wa CCM kumchagua Rashid Mohamed kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM katika uchaguzi wa uliofanyika mwezi Desemba mwaka jana.

Awali wa Sadifa alitiwa mbaroni Desemba 10 mwaka 2017  kwa tuhuma hizo na kupandishwa kizimbani Desemba 11, mwaka jana.

Shitaka la kwanza alidaiwa Desemba 9, 2017 katika makazi yake kwenye Kata ya Mnada mjini Dodoma akiwa Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM aliwahonga wanachama ili wamchague Rashid Mohamed aliyekuwa akiwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika uchaguzi mkuu wa umoja huo.

Sadifa katika shtaka la pili alidaiwa katika eneo hilo na siku hiyo hiyo, aliwaahidi kuwalipia usafiri wanachama wa umoja huo kuwasafirisha kutoka Dodoma hadi Kagera kama zawadi ili wamchague Rashid Mohamed aliyekuwa akiwania nafasi ya makamu mwenyekiti katika uchaguzi huo.

error: Content is protected !!