March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe, wabunge Chadema ‘waliamsha dude’ ofisi za Tume

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema (katikati) akiwa na Mgombea Ubunge Kinondoni, Salum Mwalimu walipowasili ofisi za NEC

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiongozana na Mgombea Ubunge Jimbo la Kinodnoni, Salumu Mwalimu pamoja na wabunge wa Chadema katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) kuhoji sababu za mawakala wake kutopewa hati za viapo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mbowe akiongozana na wenzake amelazimika kufika katika ofisi hizo kwa lengo la kuhoji sababu zilizofanya mawakala wa Uchaguzi Jimbo la Kinondoni wasipewa nakala za viapo hadi leo huku ikiwa uchaguzi unatarajiwa kufanyika Februari 17, mwaka huu.

Mwenyekiti huyo pamoja na kuongozana na Mwalimu, mgombea ubunge wa jimbo hilo, pia ameongozana na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini na mwanachama wengine wa chama hicho.

“Tumekuja Tume kuonana na Mkurugenzi wa Tume Taifa juu ya hujuma zinazofanywa na Mkurugenzi wa Kinondoni kwa kutowapa mawakala wetu nakala za kiapo mpaka sasa hivi,” amesema Mbowe.

Lakini pamoja na Mbowe na wenzake kufika ofisini hapo, wameambiwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima hayupo ofisini na wameahidi kuendelea kubaki mpaka atakaporudi ofisini.

MwanaHALISI Online itaendelea kuwapa taarifa nini kinachopendelea katika ofisi za NEC.

 

error: Content is protected !!