May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaigomea TFF, kuingiza timu saa 11 jioni

Hassan Bumbuli, Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga

Spread the love

 

MABINGWA wa Kihistoria nchini Tanzania, Yanga ya jijini Dar es Salaam umesema, utaipeleka timu yao katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, muda uliopangwa awali was aa 11:00 jioni na sis aa 1:00 usiku, leo Jumamosi, tarehe 8 Mei 2021. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Yanga wamesema, uamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wa kubadili muda wa mtanange kati ya watani wa jadi, Simba dhidi ya Yanga, ni kinyume na Kanuni ya 15(10) za Ligi Kuu inayohusu taratibu za mchezo.

Kanuni hiyo inasema “mabadiliko yoyote ya muda wa kuanza mchezo yatajulishwa ipasavyo kwa pamnde zote husika za mchezo angalau saa 24 kabla ya muda wa awali.”

Hata hivyo, leo mchana Jumamosi, wakati mashabiki wakiwa tayari wameanza kuingia uwanjani, TFF ilitoa taarifa ya mabadiliko ya ratiba ya mchezo huo kwa kile ilichoeleza ni maelekezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Taarifa hiyo ya TFF, haikufafanua zaidi sababu za msingi za mabadiliko ya mchezo huo.

Kutokana na hilo, taarifa ya Yanga, iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano imesema “uongozi wa Yanga, unapinga mabadiliko hayo hivyo, itapeleka timu uwanjani kwa muda wa awali was aa 11:00 jioni.”

“Uongozi wa Yanga unaitaka Bodi ya Ligi na TFF kuendesha ligi kwa kuzingatia na kuheshimu kanuni zilizowekwa,” imesema Yanga

error: Content is protected !!