May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba, Yanga kupigwa saa 1 usiku

Clifford Ndimbo, Msemaji wa TFF

Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeusogeza mbele, mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2020/21, kati ya Simba dhidi ya Yanga, kutoka saa 11:00 jioni hadi saa 1:00 usiku. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam… (endelea). 

Mchezo huo, unachezwa leo Jumamosi, tarehe 8 Mei 2021, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, mkoani Dar es Salaam.

Taarifa ya TFF, iliyotolewa mchana na Ofisa Habari na Mawasiliano, Cliford Ndimbo imesema, mabadiliko hayo yanatokana na maelekezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Tayari mashabiki wa watani hao wa jadi, wamekwisha anza kuingia uwanjani kushuhudia kipute hicho.

error: Content is protected !!