Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wickremesinghe aapishwa kuwa rais wa mpito wa Sri Lanka
Kimataifa

Wickremesinghe aapishwa kuwa rais wa mpito wa Sri Lanka

Spread the love

 

WAZIRI Mkuu wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe ameapishwa leo, kuwa rais wa mpito wa taifa hilo. Anachukua nafasi ya Gotabaya Rajapaksa, aliyejiuzulu wadhifa wake. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wickremesinghe atashika wadhifa huo, hadi Bunge litakapomchagua mrithi wa kiongozi huyo, kufuatia maandamano ya umma kulalamikia kuporomoka kwa uchumi wa nchi hiyo na kumlazimu kuondoka madarakani.

Spika wa Bunge, Mahinda Yapa Abeywardana amesema, Rajapaksa alijiuzulu rasmi kama rais jana Alhamisi na wabunge watakutana Jumamosi ili kuchagua kiongozi mpya.”

Nimepokea barua ya kujiuzulu iliyotumwa na rais Rajapaksa. Rais amejiuzulu rasmi kisheria 14 Julai mwaka huu.

Kuanzia sasa, mchakato wa kumchagua rais mpya utaanza, hadi mchakato huo utakapokamilika, waziri mkuu atateuliwa kutekeleza majukumu ya rais kama ilivyoainishwa kwenye katiba.”

Spika huyo amesema kuwa kiongozi atakayechaguliwa, atahudumu kama rais kwa muda uliosalia wa Rajapaksa ambao unakamilika mwaka 2024.

Ameeleza kuwa mchakato huo utachukua muda wa siku saba. Kiongozi huyo mpya pia atapata nafasi ya kumteua waziri mkuu, ambaye lazima aidhinishwe na Bunge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!