Waziri Mkuu wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe amekubali kujiuzulu baada ya viongozi wa vyama vya siasa nchini humo kumtaka yeye na rais aliye madarakani kukaa kando. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Hatua hiyo imetokana na shinikizo la waandamanaji ambao wameyavamia makazi yake na kuyachoma moto kutokana na kughadhibishwa na mdororo wa kiuchumi.
Msemaji wa waziri mkuu, Dinouk Colambage, amesema Wickremesinghe amewaambia viongozi wa chama kwamba atajiuzulu pale ambapo pande zote zitakapokubaliana katika namna ya uundwaji wa serikali mpya.
Ametoa uamuzi huo leo tarehe 9 Julai, 2022 baada ya kufanyika kwa maandamano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Sri Lanka.
Maelfu ya watu walivunja vizuizi na kuingia kwenye makazi ya Rais Gotabaya Rajapaksa na ofisi iliyo karibu kwa kuonesha hasira zao kwa kiongozi huyo.
Picha za video ziliwaonesha mamia ya waandamanaji wakiwa katika bustani yenye bwawa katika makazi hayo na wengine wakiwa na nyuso za furaha.
Leave a comment