August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yamtambulisha rasmi Bigirimana

Spread the love

 

IKIWA katikati ya mkutano mkuu wa mwaka wa klabu hiyo, ambao umebeba ajenda kubwa ya Uchaguzi, Rais mteule wa klabu hiyo Mhandisi Hersi Said alimleta mbele ya wanachama mchwzaji mpya wa klabu hiyo Gael Bigirimana raia wa Burundi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezaji huyo ambaye kwa nyakati tofauti alichezea kwenye klabu za Coventry City, Newcastle United, Rangers na mpaka anatua Yanga, anatokea kwenye klabu ya Glentoran.

Wakati wa utambulisho wake mbele ya wanachama, mchezaji huyo alikuwa ameshatinga jezi ya klabu hiyo ambayo kwa mujibu wa taarifa amefanikiwa kusaini mktaba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia Yanga, kuanzia msimu ujao wa mashindano.

Hersi alisema kuwa, klabu hiyo mpaka sasa imefanikiwa kusajili wachezaji watano, na siku ya jumatatu watamtambulisha mchezaji mwengine kutoka Afrika ya Magharibi.

“Tumeshasajili wachezaji watano mpaka sasa, na siku ya jumatatu tutamtambulisha mchezaji mwengine ambaye ni hatari kutoka Afrika ya Magharibi.” Alisema kiongozi huyo

Mara baada ya kiongozi huyo kutoa ahadi hiyo kwa wanachama, mchezaji huyo alipewa nafasi ya kuwasalimia mashabiki wa klabu hiyo na kusema kuwa yupo tayari kupambana na kwa ajili ya Yanga kwa kuwa ameshajua malengo yao ni nini?

“Nilipata ofa nyingi sana kabla kuja Yanga, tena nyingine kutoka barani Ulaya, nimamua kuja kwa wananchi mara baada ya Rais wa klabu kunipa malengo yao na hivyo nikaona ni sehemu sahihi.” Alisema mchezaji huyo

Bigirimana anakuwa mchezji watatu kutambulishwa na Yanga, toka kufunguliwa kwa dirisha kubwa la usajili Julai Mosi mwaka huu.

Wachezaji wengine waliosajiliwa mpaka sasa ni Bernad Morrison kutoka Ghana na Lazarious Kambale aliyejiunga na Yanga akitokea kwenye klabu ya Kaizer Chief ya nchini Afrika Kusini.

error: Content is protected !!